Monday, 4 June 2012

[wanabidii] Wapelelezi wa Ukoloni ulikuja na Ukristo + Warabu wakaja na Uislamu

Katika historia ya Tanzania na Africa Mashariki tunakumbuka Ukristo uliingia kabla ya ukoloni enzi za akina Vasco Da Gama mfanya biashara kutoka ureno aliefika Tanganyika na Kenya. Huyu jamaa na wenzake walioingia kwa lengo kama hilo ndipo Ukristo ulipoanza kuingia Zanzibar na baadae ukaja bara. Baada ya mkutano wa Berlin 1884-85 wakoloni walipogawana Afrika ndipo wakaja wafanya biashara, wapelelezi na wahubiri wa Ukristo. Ukristo ulienea bara kwa hali kubwa sana wakati wa ukoloni.

Historia inaonesha Waarabu kutoka Omani walimtimua Vasco da Gama na kuimiliki Z'bar na kingo za bahari kunzia Mombasa, Tanga, Dsm Lindi Mwatara.
Historia imeandika kuwa Uslamu uliingia Zanzibar, Mombasa, Tabora, Kigoma na kwengineko. Warabu hao walioleta dini ya Kiisamu ndiyo hao hao walioleta utumwa.

Natafakari kwa kina leo hii kuna watu (waafrika) tunagombania dini ambazo walizileta ndiyo hao waliwatawala babu zetu na kuwatumikisha katika mashamba yao na kupeleka bidhaa zilizopatikana Ulaya...
Wrngine ndiyo hao waliouza babu zetu na kama bidhaa?

Baadhi ya Wanzibar wametokea Geita, Tabora, Kigoma, Bagamoyo.... Wanataka kujitenga kwa lipi wakati chimbuko lao nu huku bara?
Hao waliotuminisha katika dini zao waliuza babu zetu kama bidhaa, wengine waliwaua, wangine wakatumikisha kujenga reli na majumba yako kama ofisi....

Kwa nini twagombania dini za watu walitunyonya kwa kuchukua rasilimali na wengine kutupiga mnada kama bidhaa??

Tutafakari na kufanya maamzi ya busara kabla ya kugombana
  

0 comments:

Post a Comment