Napenda kujuzwa kwani ni siku nyingi zimepita tokea nifanye mtihani wa mwisho wa NECTA.
Wakati nafanya mtihani wa mwisho nikiwa kidato cha sita tulikuwa tunaandika Namba katika fomu zetu za kufanyia mitihani.
Hivi karibuni nimesikia tamko kutoka kwa moja ya makundi ya dini ya kiislamu wakilalamika kuwa wanafelishwa na NECTA.
Nimejiuliza hivi taratibu za kuandikisha mitihani zimebadilika? Yani siku hizi watahiniwa huandika majina yao badala ya namba?
Na kwa kuwa huo ndiyo ukweli nataka basi hija hiyo inaweza kuwa justifiable?
Otherwise kama bado watu wanaandikisha namba juu ya karatasi za mitihani basi waliotoa hoja hiyo wanaweza kuwa kwenye kundi
alilosema raisi wa awamu ya tatu kuwa Watz nadhani baadhi si wote ni wavivu wa kufikiri. Hao wanaotoa hoja ya kama hiyo kwanza walitakiwa waje na scientific justifiable research kutuhakikishia hilo wanalosema na kutoa tamko mbele ya dunia.
0 comments:
Post a Comment