Monday, 4 June 2012

[wanabidii] MFUMO DUME = MFUMO KRISTO?

Katika karne iliyopita tumeshuhudia wanawake pamoja na makundi mengine ya wanaharakati wakidai kwa nguvu sana usawa, upendeleo na haki ambazo wanadai zimeporwa na wanaume,
Pia walidai kuwa mfumo dume ndo unaowadidimiza wanawake katika elimu, biashara, nafasi za kazi na siasa.
Tumeshuhudia hata serikali yetu ikitenga viti vya ubunge vya bure/ upendeleo kwa wanawake angalau wafikie asilimia 30%, kwa sasa nimewasikia baadhi ya wanawake wanataka iwe 50% kwa 50% ya ubunge wa Tanzania.
Pia serikali iliamua kuwapendelea wasichana kwenye elimu kwa makusudi kabisa, mf; kama mvulana amepata division 2 na msichana division 3 na ikawa hiyo nafasi inagombewa na wote wawili basi atapewa msichana kwa kumpendelea na kijana wa kiume ataachwa.
Siku hizi kuna upendeleo mwingi tu kwa wanawake ili kuinua ustawi  wao katika nyanja mbali mbali, pia kuna wizara ya wanawake, watoto nk.
Wameanzisha Bank yao ya wanawake nk,
Huo nao mi ninauita ubaguzi wa usiku, namaanisha hauonekani kirahi sana, maana kama binadamu wote ni sawa iweje mwingine apendelewe na mwingine aachwe?
Sasa kila kundi limeibuka linataka haki zake na pia nafasi za upendeleo katika bunge na maeneo mengine ya kijamii. walemavu, mashoga, kulima, wafugaji yaani orodha ni ndefu.
Pia kuna watu wamekopi na kupaste aina hiyo ya uana harakati baada ya kuona wanawake wamefanikiwa na wanapewa upendeleo.
Wao wamekuja na kauli mbiu ya kuwa nchi hii inaongozwa kwa mfumo KRISTO.
Kwa hiyo nao wanataka haki sawa, kwamba uwaziri ugawanywe sawa kwa sawa, wakuu wa mikoa na wilaya sawa kwa sawa, ufaulu wa wanafunzi sawa kwa sawa, nafasi za kiuongozi sawa kwa sawa na mengineyo meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeengi.
Tusipoangalia hata majambazi nayo yatataka haki zao, makahaba nao watataka haki zao, wavuta bangi nao watataka haki zao, ili mradi kila mtu au kundi litadai lipewe haki sawa.
Huu nao ni ubaguzi wa usiku, kutazama mambo kwa kuhisi kuonewa hivyo kulilia lilia tu ili upate huruma za watu na ukifanya uhalibifu uhurumiwe eti kwa kuwa unaonewa na kitu kisichokuwepo (cha kufikirika tu)

Kama wanawake walikuja kupambana na mfumo dume wakahurumiwa na kufanikiwa naomba wengine msikopi na kupaste kuwa sasa mnapambana na mfumo kristo mkazani mtafanikiwa.
Huo mfumo kristo haupo, mtakuwa mnapigana na kivuli ambapo mtaishia kuchoka tu au kumwaga damu na mwisho wa siku msimwone huyo adui yenu.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment