PROGRAMU 5 ZA KULINDA KOMPYUTA YAKO
Katika somo hili nazungumzia zaidi programu ( software ) zinazoweza
kutumika katika ulinzi wa kompyuta yako dhidi ya uhalifu au njia
nyingine za kuweza kuuingilia kwa mtandao au kwa kutumia vitu kama cv/
dvd na vitendea kazi vingine .
1 – ANTIVIRUS
Antivirus ni programu inayoweza kuingizwa kwenye kompyuta kwa nia ya
kuilinda dhidi ya mashambulizi ya virus kwa njia ya mtandao au kwa
njia ya kuchomeka vitu , duniani kuna antivirus za aina mbalimbali na
nyingi zinavitu vinavyo fanana .
Pendekezo la Antivirus
AVAST 7 – Napendekeza Avast 7 kwa sababu unaweza kuitumia ukiwa kwenye
safemode ambapo programu nyingi hazifanyi kazi ,inafanya kazi na
programu zote , unaweza kuitumia kusafisha virus kwa njia ya DOS na ni
programu inayofanya kazi kwenye kompyuta nyingi zenye uwezo mdogo
chini ya MB512 za RAM.
Kuna AVAST 7 Antivirus Free ambayo ni ya Bure (Huria ) sema unatakiwa
uisajili kabla ya siku 30 upate siku 365 za utumiaji lakini pia ni
bure , kuna inayouzwa ambayo ni Proffesional na Internet Security
kwahiyo ni wewe mwenyewe kuchagua .
2- INTERNET SECURITY
Internet security ni kama antivirus sema kuna baadhi zenye vitu vingi
zaidi kama firewall ,antispyware na programu nyingine zinazoweza
kutumika kukuepusha na madhara kwa njia ya mtandao .
Kama wewe ni mtumiaji sana wa mitandao na unatembelea tovuti
mbalimbali na kompyuta yako inauwezo na mwendo mkubwa unaweza kutumia
Internet security Kaspesky 2012 .
Tatizo la kaspersky ni
Ni Programu inayotakiwa kuboreshwa mara kwa mara na Updates zake ni
kubwa kiasi kwamba zinawashinda watu wa kawaida kutokana na gharama za
mtandao .
Huwa inasumbua kwa watu waliokuwa kwenye ( LAN) wanaoshirikiana katika
kufanya kazi pamoja au kushare taarifa na kuzifanyia pamoja na kama
kuna programu za uhandisi kama Autocad ,Archicad na nyingine nyingi
huwa zinasumbua kufanya kazi pamoja na kaspersky kwa njia ya mtandao
wa LAN
Hakuna Programu ya Kaspersky ambayo ni ya bure ( Huria ) zote ni
lazima ununue au unapewa siku 90 kwa ajili ya majaribio .
3 -FIREWALL
Firewall ni kama ukuta kati ya kompyuta yako na nyingine zilizojaa
duniani , kwa kawaida kila kompyta yenye windows ina firewall lakini
wengi wanapenda kuidisable hii ili uweze kufanya kazi vizuri na
programu nyingine haswa internet security zinazokuja na firewall
zake .
Unatakiwa uwe makini unapotumia au kuweka firewall katika kompyuta
yako , kama nilivyosema huu ni ukuta ukiweka vibaya bila kusoma
maelezo unaweza kufunga programu zako unazotumia zisifanye kazi au
unapojaribu kuweka programu nyingine inaweza isiweze kuingia kutokana
na maelezo uliyoipa firewall yako .
Pendekezo zuri la Firewall ni ZoneAlarm hii ina matoleo ya Bure
( Huria ) na ya kununua
4 -ANTISPYWARE
Antispyware iko kwa ajili ya kukulinda dhidi ya spyware . spyware ni
programu zilizojaa kwenye mitandao zenye lengo/nia/kazi ya kuingia
kwenye kompyuta nyingine na kuhamisha taarifa au nyaraka kwenda maeneo
mengine ( kuiba )
.
Tatizo la spyware sio kubwa sana kwa kipindi cha sasa hivi haswa kwa
watumiaji wa windows xp sp3 na kuendelea .
Pendekezo la Antispyware ni Lavasoft Antispyware na ArafaSoft.
Ukiwa na antivirus , internet security , antispyware na firewall
unaweza kujilinda dhidi ya mashambulizi mengi .
Huwezi kujihakikishia ulinzi kwenye kompyuta yako kama programu zako
za antivirus , internet security , antispyware au hata firewall
hazijaboreshwa kwa kufanya updates za mara kwa mara angalau mara 1 kwa
wiki Kutegemeana na Matumizi yako kwa njia ya mtandao na jinsi
unavyoingiza na kutoa vitu katika mashine yako .
Ili kuweza kujihakikishia usalama zaidi ni vizuri programu zako ziwe
zimesajiliwa na kuwa na leseni ili kuweza kupata huduma bora zaidi
kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa hizo .
Programu nyingi tajwa hapo juu zinaweza kujiboresha ( Update) zenyewe
automatic ukiunganishwa tu na mtandao lakini pia unaweza kuziboresha
kwa njia nyingine (Offline) hii inatumika kwa watu ambao hawana huduma
za mtandao au wana mashine nyingi lakini wanapenda kuzifanyia
maboresho kwa pamoja .
JINSI YA KUBORESHA MASHINE NYINGI KWA WAKATI MMOJA .
Programu nyingi zinakitu kinaitwa (OFFLINE UPDATE )katika tovuti za
watengenezaji wa bidhaa husika .
1- Download ( Shusha ) Offline Update toka kwenye tovuti za pragramu
husika
2- Hifadhi kwenye kifaa kama cd au DVD ( Usitumie Flashdisk kwa
sababu inaweza kuambukiza virus toka komputa moja kwenda nyingine
labda kama unaamini hakuna tishio hilo )
3- Unatakiwa ujue Sehemu Ambayo Update inakaa
inayohusiana na Programu hiyo , unaweza kupaste hiyo File ya update
uliyoshusha kwenye mtandao – Njia ya tatu inatumika kama mashine yaani
komputa ziko mbalimbali na hazijaunganishwa .
4- Kama mashine zako zimeunganishwa kwa kutumia cable ndani ya ofisi
moja basi unatakiwa kutengeneza folder moja labda katika server au
popote ambapo file hilo linaweza kukaa kisha ukaamuru mashine nyingine
zote kuchukuwa updates zake kwa kiunganishi ulichoweka .
NJIA HIZI NI GHARAMA NAFUU KWA WALE WANAOPENDA GHARAMA NAFUU ZA
MATUMIZI YAO YA MAWASILIANO NA PIA HAIWEZI KURISK KOMPUTER HIZO
KUVAMIWA AU KUIBIWA TAARIFA PINDI ZINAPOUNGANISHWA KWA NJIA YA MTANDAO
MUDA MWINGI .
5 – KULINDA KOMPUTER DHIDI YA REMOVABLES
Nimetumia Removables kwa kumaanisha vitu unavyoweza kuingiza ,
kuchomeka na kuchomoa kwa ajili ya kuhamisha data , programu au
chochote kati ya komputer na vifaa vingine .
Ukiacha kwa njia ya Mtandao ambayo inaweza kulindwa zaidi na Settings
na Ubora wa programu unazotumia kuna hizi nyingine ambazo mtu anaweza
kuchomeka flashdisk akahamisha vitu , au cd akaweza kuandika data na
kuondoka nazo .
Unaweza kuficha CD/DVD Drive isionekane au isiweze kutumika kwa
kutumia programu za komputa hadi hapo unapotaka kutumia wewe
mwenyewe , moja ya programu hii ni Arafasoft system optimiser 6.0
sehemu ya Privacy Tools .
Tafadhali usitumie programu zinazokuja na External HardDrive au
Flashdisk kuweka Lock maana zinaweza kuchagua na kuharibu mfumo wa
Komputer yako au kama programu hiyo ikiharibika unaweza kupoteza
taarifa zako , tumia programu huru ambazo zinaweza kufanya kazi kwenye
kifaa chochote kinachochomekwa .
Somo hili ni kwa ajili ya kujifunza tu , unaweza kupata maarifa zaidi
kwa kusoma zaidi kwa njia ya mtandao na kufanyia majaribio ya vitendo
au hata kwa kuuliza .
Ukitumia vibaya unaweza kupoteza taarifa zako na kutishia maumivu
mengine dhidi ya vifaa vyako , kama unatumia ni bora uwe unajua
unachofanya .
By YONA F MARO
+255786 806028
Thursday, 07 June 2012
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment