Friday, 22 June 2012

[wanabidii] KADA CHADEMA, KADA CCM

Wataalam,

Nafuatilia mjadala uliopewa kichwa cha habari KAULI YA JOHN MNYIKA. Kwa hakika michango ya tulio wengi inaegemea katika upenzi, ushabiki, unazi wa vyama. Ni kukabana koo mradi ionekane chama chako kiko sawa hata kama si kwa hoja madhubuti. Bahati mbaya sana wengi wanasema hawana vyama na wala hawaegemei upande wowote.

Ningependa tu kushauri kwamba ni vizuri tukasema kwa uwazi (Declare Conflict of Interests) ili kwa vyama tunavyoshabikia mwanzoni kabisa mwa kila topic tunayotaka kuchangia. Mfano mzuri ni Tumaini Makene (CHADEMA), naamini pia labda na Yona Maro (CCM) maana michango yao inaonesha mwelekeo wa moja kwa moja kwa vyama vyao.

Naomba kutoa hoja.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment