Tuesday, 3 July 2012

[wanabidii] Misahama ya ya kodi Trillion 5; Bajeti ya Mishahara 3.5 Trillion

Kwa mujibu wa Mbatia leo bungeni anaishangaa serikali jinsi inavyodai haina hela za kulipa mishahara mizuri wakati imesamehe kodi kwa kiasi cha zaidi ya Trillion 5 na ushei.

Hela za kuwalipa wabunge zipo, mishahara minono na posho, magari ya anasa na ofisi za kifahari kwa tume ya katiba zipo
Mishahara ya kuongeza ulaji kwa Ma-RC wapya, ma-DC wapya ya sekretarieti mpya za mikoa na wilaya zipo.

Kulipa watumishi kima cha chini hela hamna, kulipa walimu madai yao hela hamna, kulipa ma-dk hapo ndiyo serikali haina uwezo.

Raisi kwenda nje ya nchi kwa ziara zisizo na tija heli ipo. hela za kuibwa na watendaji wa halmashauri zipo. 
Napata tabu kidogo ninaposikia hela hamna kwa baadhi ya watu ila zipo kwa wateule wachache.
Tz ya CCM inafanya vitu vya kushangaza kweli jamani

0 comments:

Post a Comment