Friday, 6 July 2012

[wanabidii] MAONI YA MHE BERNARD MEMBE KUHUSU SAKATA LA MELI ZA IRAN

Serikali imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha
bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo. Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili
zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha. Tanzania imewaarifu nchi
zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na
kushirikiana kuthibitisha taarifa hii. Tumefanya hivyo kwa kuzingatia
uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa
kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa. Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala
wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran,
Balozi wa Iran nchini aliitwa akakanusha. Tutakapopata matokeo ya
utafiti na ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara
moja. Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli
hizo. Tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio
1920 la UN Security Council.Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani.
Tunafurahia mahusiano yetu na nchi zote duniani. Hili ni jambo
linalogusa maslahi ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani
(Muungano), tujihadhari na namna tunavyolizungumzia. Tusimame pamoja
kama taifa. Nchi kwanza!

Chanzo : http://www.facebook.com/pages/Bernard-Kamilius-Membe/204958252852114

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment