Wednesday, 27 June 2012

[wanabidii] TUNALAANI KUTEKWA , KUPIGWA NA KUUMIZWA KWA DR ULIMBOKA

Ndugu zangu

Watanzania wapenda amani , utulivu , uhuru na mabadiliko popote
mlipo .

Kuanzia usiku wa jana muda wa saa 6 hivi , Taifa letu limeanza
kuandika historia mpya baada ya kutekwa kwa Dr Ulimboka ambaye ni
Kiongozi wa chama cha madaktari Tanzania na ambaye aliongoza mgomo wa
kwanza wa madaktari kote nchini .

Dr Ulimboka alipigiwa simu na mtu aliyekuwa anawasiliana nae mara kwa
mara baadaye alitekwa nyara na watu wasiojulikana na kuondoka nae
usiku huo huo bila ya taarifa zozote .

Daktari huyu amepatikana maeneo ya Bunju akiwa amepigwa vibaya na
kupatikana na majeraha sehemu kadhaa za mwili wake na sasa hivi yuko
wodi ya MOI kwa ajili ya matibabu zaidi lakini hali yake bado ni mbaya
na hawezi kuzungumza chochote .

Tunalaani kabisa kitendo hiki cha utekeji nyara wa mtu asiyekuwa na
hatia kisha kumdhuru kwa nia ya kuondoa uhai wake .

Vitendo hivi ni vigeni kabisa miongoni mwa watanzania haswa wa kizazi
cha sasa ambao wamezoea kuishi kwa kuaminiana na kwa ujirani mwema kwa
kipindi kirefu .

Pamoja na kulaani hivyo tunaomba mamlaka husika yaani serikali
kuchukuwa hatua kali dhidi ya watekaji nyara hao walioendesha kitendo
hiki kwa kuanza na kujua wale aliowasiliana nao mara ya mwisho mpaka
kumpeleka huko alikofanyiwa hivyo .

Kwa tekinologia za sasa tunaamini ushahidi mwingi umeshajiweka wenyewe
hadharani ni jukumu la serikali na wadau wengine wa ulinzi na usalama
kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya
sheria .

Mwisho tunaomba wananchi haswa madaktari waache mgomo na waendelee na
kazi zao bila hofu yoyote na kama kuna majadiliano yoyote yafanyike
kwa njia za amani na kwa muda wa kazi sio kutafutana usiku au baada ya
kazi ili kuleta usalama na kuaminiana.

Yona F Maro

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment