Saturday, 2 June 2012

[wanabidii] SIKU YA KUTOTUMIA TUMBAKU DUNIANI

Ndugu Wanabidii,

Naomba niwashirikishe hii mada, ambayo n aamini ni muhimu kwa afya ya jamii.

Tarehe 31 Mei ya kila mwaka, ni siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani. Shirika la Afya Duniani, lilichagua siku hii, baada ya kutambua kuwa janga la matumizi ya tumbaku linazidi kuangamiza dunia. Ni siku ya kutafakali juu ya madhara yanayotokana na matumizi ya tumbaku; biashara ya makampuni ya tumbaku ambayo yamedhamiria kuliangamiza dunia na jinsi ya kupambana na yote haya.

Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni "Dhibiti Makampuni ya Tumbaku, Yasiingilie Juhudi za Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku". Kauli mbiu hii ilichaguliwa, baada ya kutambua ongezeko la njama za makampuni ya tumbaku, kuzuia sera nzuri za kulinda afya ya jamii dhidi ya matumizi ya tumbaku.

Tanzania Tobacco Control Forum (TTCF), ikishirikiana na wadau wengine tuliadhimisha siku hii, pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Maduhumuni ya kuchagua mahali pale, ni kutoa dukuduku zetu, jinsi makampuni yalivyougeuza uwanja ule "mtego wa kifo" (death trap) kwa kurudisha uvutaji wa tumbaku, ambao ulishazuiliwa tangu mwaka 2007. Tafadhali soma "attachment" ya "Press Release" niliyoitoa siku moja kabla.

Pia naomba niwafahamishe kuwa, kilimo cha tumbaku huathiri mkulima kiafya na kiuchumi, huaribu ardhi na vyanzo vya maji na kusahababisha majangwa kwa ukataji miti mingi sana ya kukaushia tumbaku. Tumekuwa tunajitahidi sana kuhamasisha wakulima wajikite kwenye mazao mbadala, na kule Namtumbo, wakulima wengi wameweza kujikwamua. Wakati tukifanya hivyo, makampuni yamekuwa yanafanya kila hila, kutoa taarifa za uongo kuhusu wakulima wa tumbaku na mazao mbadala. Makampuni yana chama chao, International Tobacco Growers Association (ITGA), ambacho hukitumia kudanganya kwa kujifanya kuwasemea wakulima. Mliosoma baadhi ya magzeti, mtakuwa mmeona walivyoandika, tena wakaitoa Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani, wakilalamikia Mkataba wa Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wa Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku; ibara ya 17 na 18, inayoziagiza Nchi Wanachama, kuwasaidia wakulima wa tumbaku na wengine wanaofanya kazi za tumbaku kupata mazao na kazi mbadala wa tumbaku. Makampuni yanafanya hivyo, kwa vile mwaka huu November kwenye WHO Conference of the Parties zitapitishwa kanuni za  ibara za 17 na 18; nia ya makampuni ni kuzuia  jitihada hizi.

Sisi tunasema, mwenye macho haambiwi ona, na mwenye maskio haambiwi sikia; wakulima wa tumbaku wana taabu sana, wanahitaji kusaidiwa; pia nchi inaanamia kwa uharibifu wa kilimo cha tumbaku, inabidi tuilinde.

Tunashukuru Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, wamesikia kilio chetu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na viwanja vyote nchini, vitaendelea kuwa bila moshi wa tumbaku asilima 100 (100% Smoke-free airports).

TUMBAKU HUUA WATU MILIONI SITA KILA MWAKA DUNIANI WANAOVUTA, NA WENGINE LAKI SITA WANAOVUTISHWA MOSHI WA TUMBAKU. Tusaidiane kukomesha vifo hivi ambavyo vinazuilika.

Nawawekea na baadhi ya picha za maadhimisho.

Pia namshukuru bwana David Chikoko kwa katuni nzuri

LKK
 
Lutgard Kokulinda Kagaruki
Executive Director
Tanzania Tobacco Control Forum
P. O. Box 33105
Dar es Salaam, Tanzania
Tel: Off. +255 732 924088
Tel: Mob. +255 754 284528
Fax: +255 22 2771680

0 comments:

Post a Comment