Friday, 1 June 2012

[wanabidii] Mbowe akemea propaganda za udini, ukabila

Wanabidii, Salaam.

Nipo Newala Mtwara na leo jioni nimehudhuria mkutano wa hadhara wa Chadema umehutubiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Moja ya yaliyonivutia katika hotuba hiyo ni karipio lake kuhusu propaganda za udini na ukabila.

Akasema propaganda hizo zinafanywa hasa na watawala ili kuigawa jamii na kuitawala kirahisi, lakini akaonya kwamba inachochea mgawanyiko na kwamba hata machafuko yanayotokea Zanzibar kwa kisingizio cha kupinga Katiba Mpya, ni kukua kwa athari za propaganda za udini na ukabila.

Lakini kimsingi mkutano ulihudhuriwa na watu wengi sana na jioni ya leo palikuwa na mijadala maeneo tofauti ya Newala kuhusu ujio wa Chadema.

Ninawasilisha

Mnasemaje?

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment