Tuesday, 26 June 2012

[wanabidii] Rais Jakaya Kikwete na Uthibiti wa Mkoa wa Mbeya

Ndugu zangu

Kama mnavyokumbuka kuna kipindi rais wa tanzania aliwahi kufanya ziara
katika mkoa wa mbeya na msafara wake kupopolewa na mawe na baadhi ya
wananchi wa mkoa huo , baadaye ikasikika kwamba wale watuhumiwa wa
kisa hicho walikamatwa lakini usikilizaji wa kesi zao umeonekana kuwa
kimya mpaka leo wengi wetu hatujui kilichoendelea baada ya hapo .

Umepita muda mrefu bila Rais kikwete kutia mguu tena mkoa wa mbeya na
hata mikoa jirani hali inaoonyesha kuna mambo yanayoendelea ambayo
watanzania wengi hawayajui na ambayo yanaweza kufikisha nchi hii haswa
ukanda wa mkoa wa mbeya na mengine katika hali mbaya mbeleni .

Mimi nashauri rais , washauri wake na wadau wengine wa maendeleo
kuangalia ukanda huu kwa jicho pevu na kuacha chuki za kisiasa au visa
vingine vya nyuma , wafikirie kujenga mkoa huu na mengine ya jirani na
iwe inatembelewa mara kwa mara na viongozi wa kitaifa .

Rais jakaya mrisho kikwete ni rais wa watanzania wote waliomchagua
hata kama baadhi ya maeneo alipata kura chache au vipenzi vyake
havikupita hizo sio sababu za kuendeleza mambo haya hata katika
utendaji wa kila siku wa shuguli za kujenga nchi .

Tunataka rais kikwete aangalie eneo hilo kurudisha udhibiti na hali ya
kuaminiana watu wafanye shuguli zao .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment