Wanabodi!
Nimepokea kwa masikitiko makubwa tena nichukue fursa hii KULAANI kitendo kilichofanywa na watu wasiojulikana vizuri bado kwa Dk Ulimboka wa Chama Cha Madaktari Tanzania. Najaribu kutafsiri haraka kuwa huu yawezekana ni mchezo mchafu sana uliochezwa na watu wasio upande wa kutaka kujua shida za wananchi, na matatizo yanayowakabili kwa nia ya kutaka kuwatisha wengine. Bahati mbaya sana tukio hili limetokea katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari unashamiri (My goodness).
Imenijia kwenye akili kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kwa sasa tukio hili likawaunganisha watu zaidi, maana inaonekana ni uonevu wa dhahiri. Kwa sababu Dk. Ulimboka ni Public Figure ni vema sana kwa Serikali kutolea tamko tukio zima hasa katika kipindi hiki ambacho Bunge la Bajeti linaendelea otherwise, tafsiri ya tulio wengi itakuwa dhidi ya Serikali. Na kwa kweli maneno ya kutumika katika tamko hilo yawe makini sana maana nimesoma kwenye vyombo mbalimbali na mitandao ya kijamii kuwa kiongozi mmoja mwenye dhamana kubwa kasema eti MGOMO WA MADAKTARI - LIWALO NA LIWE huku mkuu wa kaya naye akijiandaa na safari yake ya Canada.
Please, Madaktari wasikilizwe kwanza kuondoa matatizo.
Tony
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment