Ndugu zangu,
Mara nyingi nimekuwa nikisikia kuwa serikali yetu ni sikivu!
Naishangaa kauri hii kwasababu inatoka bila kusema imeskia nini hata
serikali yetu ijiite ni sikivu.
Madaktari wanalia, wagonjwa tunaotetewa kuwa kwa mgomo wa madaktari
tutakufa tunalia kwa kuambiwa tukanunue dawa na vifaa vya tiba, walimu
wanalia, wanafunzi wanalia kwa kukosa madawati na vifaa vya
kufundishiwa, wanafunzi waliomaliza masomo wanalia kwa kukosa ajira,
wastaafu wanalia kwa kukosa malipo yao ya uzeeni, wazee wa iliyokuwa
Afrika Mashariki wanalia, watumishi wengi wa umma wanalia kwa madai
mbalimbali serikalini, wananchi kwa ujumla tunalia kwa jinsi maisha
yalivyo magumu katika nchi yetu yenye kila aina ya utajiri bila
serikali kujua kwanini wananchi ni masikini, n.k! Usikivu wa serikali
yetu ijiitayo sikivu, uko wapi katika vilio hivi?!
Kwa matokeo ya mitihani ya wanafunzi wetu mashuleni siku hizi, hakuna
awezaye kubisha kuwa huenda hayo ni matokeo ya mgomo wa chini kwa
chini wa walimu wanaolia bila kusikilizwa na serikali yetu ijiitayo ni
sikivu!
Hapo, ndipo nikasema je; serikali yetu ijiitayo ni sikivu ili ifurahi
inataka madaktari nao wagome mgomo wa chini kwa chini kama walimu na
matokeo ya mgomo huo wa chini kwa chini wa madaktari yaonekane kama
yanavyoonekana matokeo ya mitihani ya wanafunzi wetu wengi wa siku
hizi?
Na kama serikali yetu ijiitayo ni sikivu ndivyo inavyotaka kuwa kila
kundi linalo lialia liwe linaendesha mgomo wa aina ya walimu, je;
inajua athari yake kwa taifa? Athari yake kwao wachache wasio lia?
Tunajenga taifa gani kuwafanya watu kulialia hovyo huku ukiwataka wawe
wakikwambia hakuna matatizo wakati watu wakiumia na taifa kuangamia?!
Tuache unafiki, serikali yetu ni kama kivuli ndio maana haiwezi
kusikia vilio vya watu wake japo ina masikio! Tunataka dawa
hospitalini ili tukipata tiba thabiti tujenge taifa letu tukiwa na
afya njema, wao wanajenga barabara! yakuitumia nani? maiti? Hivi ukiwa
mgonjwa mahututi au maiti, utaona uzuri wa barabara
uipitayo/kupitishwa?!
Madaktari hamko peke yenu mnaolia dhidi ya serikali hii, tupo wengi!
Naichukia serikali ijiitayo sikivu wakati haina inachokisikia! Nawapa
pole wahanga wenzangu wote mnaolia pamoja nami.
Nampongeza Mh. Mnyika kwa kusema ukweli mbele ya Tanzania (bungeni)
kuwa "Rais Kikwete ni DHAIFU", huo ni ukweli nami nauunga mkono.
Nawapongeza madaktari kwa kutokuwa wanafiki kulia waziwazi bila kulia
chini chini ambapo athari zake ni kubwa kuliko waliavyo sasa kwa
mgomo!
Muhimu, wote tunaolialia hivi dhidi ya serikali yetu ambayo tumeiweka
wenyewe madarakani, tutaendelea kulialia hivi mpaka lini? Tukiweza,
tutafari na tuchukue hatua!
Asante.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment