Kwenu Viongozi Gymkhana Club
Mndengereko mmoja alipata kusema kwa lugha yake " Changes are inevitable" na mhehe fulani akaongezea " Changes are Painfully". Lakini Ukienda darasani Changes zina stages zake ili uweze kufanikiwa. Inategemea unatumia aina gani ya changes. Wiki iliyopita nilitembelea mahali ambapo ndio msingi wa mimi kuwa hapa nilipo nikakutana na vitu vya ajabu sana. Niliingia Gymkhana Club nikaenda mens bar nikakuta wahudumu tu hakuna hata member mmoja. Nikaenda kwa manji (Restaurant) nikamkuta amelala na hakuna watu kabisa. Ikabidi niulize Jamani kulikoni. Ndio nikaambia kuna mabadiliko ndugu uongozi mpya na mambo mapya. Sikujali sana ila kitu kilichoniuma ni kufukuza watoto wa wafanyakazi na wanafunzi wa shule mbali mbali ambao walikuwa kwenye training mbali mbali kama za golf na tennis kisa sio members.
Wakati Captain Malinzi anaingia mwaka 2006 alikuta Tanzania ina Golf Professional Wawili tu Salim Mwanyenza na Juma Mrami. na wa tatu alikuwa ni Davis ambaye yeye alikuwa based sana Mombasa. Hivyo Captain Malinzi Akaanza na Program za kutrain vijana na mpaka anaondoka madarakani amecha professional zaidi ya kumi. Hawa professional wote ninaowasema ni watoto wa maskini au Caddies hakuna mtoto wa tajiri hata mmoja. Ma pro wengi wa golf east , southern and central africa ni macaddy by origin. Nenda south africa, zimbabwe na sehemu yoyote unayoijua Caddies ndio professional wa Golf Sehemu mbali mbali duniani baada ya kuwa promoted kutokana na mashindano mbali mbali na uwezo wanaouonyesha. Ma pro wote wa tz walikuwa macaddy . Sasa leo hii kuwafukuza wanafunzi na watoto maana yake unataka mchezo wa golf na tennis uendelee kuitwa wa wazungu na matajiri tu. Ilichukua miaka mingi golf na tennis ( Gymkhana Club) kuwa club ya weusi ilikuwa ni ya wahindi na wazungu tu mswahili alikuwa mr george christos. Alipoingia Retired Lietenant G Sayore akaanza kubadilisha mchezo wa golf kutoka uzungu na uhindi na kuwa wa watu weusi. Alijitahidi kuwaleta viongozi wengi na wakubwa wengi ambao ni waswahili kwani kulikuwa na waswahili wachache sasa wanaocheza golf. Kutokana na members watoto wao wanacheza golf as leisure ukaandaliwa mpango kabambe wa kutayarisha vijana ili wawe wachezaji wazuri wa baadae yaani Golf junior academy ambayo inaudhamini kutoka st Endrews na Kwa watu mbali mbali ambapo washiriki ni watoto wa wafanyakazi na wanafunzi wa shule mbali mbali za msingi na sekondari. Sio golf tu tenis na creket wana juniors academy zote zimepigwa marufuku kisa wanaofundishwa sio watoto wa matajiri.
Kali kabisa Hakuna mtu yoyote hata atoke wapi atakaye ruhusiwa kuingia club mpaka awe na mwenyeji na alipe kiingilio cha shilingi elfu kumi. Na akitaka kucheza mchezo kama golf lazima awe na mwenyeji pia na alipe green fee Tshs 80,000 . Achilia mbali vifaa vya golf vya kukodi na caddy fee. Gymkhana inapokea wageni mbali mbali kwa ajiri ya mchezo wa golf na tennis mpano: marubani wa ndege za kimataifa; watalii na maofisa ubalozi na wengine wengi ambao wanapenda kucheza michezo pasipo kuwa members kwa kulipa viingilio na kucheza mchezo wanaotaka. Kwa changes hizi mpya Gymkhana imekuwa Tupu na kimya. Na hicho kinapelekea waajiriwa na wasio ajiriwa ( macaddy) kufa njaa. Ukiachilia mbali maendeleo ya club sijui nini hatima yake. Msisahau Gymkhana ni Non Profit Organization. Wasi wasi wangu ni kuturudisha enzi zile za gymkhana ya wazungu kila race na bar yao na choo chao. Members mko wapi tunaua michezo wakati ndio kauli mbiu ya serikali kwa michezo kwa watoto na vijana. Mzee andanenga anamalizia kwa kusema" Kila unachotizama , usione ukadhani. Usione jicho kutazama ukafikiri linaona" . Jamani hii ni tafsiri yangu wakati wengine wanaenda club as leisure wengine ndo watoto wao wanenda shule na nyumbani sufulia zinachafuka.
Wenu
XAVERY LANGA KAPECHA NJOVU
FORMER CADDY
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment