Wednesday, 13 June 2012

[wanabidii] FEDHA ZA ZIARA ZA JK ZAIBWA.

Maofisa watano wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa kwa ajili
ya safari za raisi.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya ikulu na wizara hiyo zimesema kwamba
maofisa hao akiwemo
mkuu wa itifaki
walifanikiwa kuchota 3 bilioni kutoka bank moja nchini.

Fedha hizo zilikuwa
zitumike kugharamia
matumizi ya safari
mbalimbali za rais. Maofisa waliotajwa katika kashfa
hiyo ya ufisadi ni mkuu wa itifaki Anthony Itatiro,
wengine ni Shamim khalifa, kaimu mhasibu mkuu
Kassim laizer, mhasibu Deltha mafie na karani wa
fedha Shaban kesi, Wote wamesimamishwa
kazi yapata wiki mbili sasa kupisha uchunguzi.

Mtoa taarifa amesema
"fedha hizo zimeibiwa kwa ustadi mkubwa, walikuwa
wametoa fedha zote banki, sijui ilifichukaje wakati
wameshapanga jinsi ya kugawana"
Taarifa nyingine
zilizopatikana zilisema katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni sefue
ameunda tume ya
kuchunguza na kuipa muda wa hadi julai 4 kukamilisha uchunguzi na kumkabidhi
ripoti.

Chanzo. Mwanahalisi
jumatano, juni 13 - 19 uk 6.


--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
+255 (0) 713 (784) 24 67 64.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment