Saturday 7 July 2012

[wanabidii] Ushauri wa mbowe juu ya msongamano wa magari

Nimesoma katika magazeti kuwa Mbowe katoa mapendekezo kadhaa juu ya kupunguza msongamano wa magari dar, baadhi ya point nilizoona ni;
1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
 
2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
 
3. Yajengwe madaraja ya watembea kwa miguu.
 
Labda namie niseme;
1. Kuwekwa ada za magari kuingia mjini
Tayari ada zipo kwa jina la "parking fee" lakini haijasaidia, kuiongeza ni kumuumiza binti anaetumia usafiri wake kwenda kazini achilia ka mkopo ka benki anakokalipa kwa shida. Kwa maana nyingine anasema watu wanaendesha magari kwenda mjini kwa ufahari, la hasha adha za daladala ndo zinasukuma, wengine ni wafanyabiashara hubeba mauzo. labda angeshauri makampuni kama NSSF na PPF waache kujenga business complex katikati ya mji. maeneo ya mlimani city na mawasiliano house hayapo azikiwe mbona yanafanya biashara vizuri tu.
 
2. Ziachwe njia za watembea kwa miguu
Sidhani kama unaweza egesha gari yono watalifunga mnyororo na kuliburuza. hata hivyo hakuna mtu anaweza tembea kwa miguu kutoka mwenge hadi posta kama tukiondoa haya magari anayozungumzia bwana mkubwa. Ningeshauri sumatra waweke madaraja ya usafiri yenye nauli tofauti mfano economy coaches (nauli 300/=) business coaches (nauli 1000/=) executive coaches (nauli 5000/=) mkazi wa makongo juu anaweza kuegesha gari mlimani city then anapanda bus hadi posta.
 
3. Kujenga madaraja ya watembea kwa miguu
Bado viwete na wasukuma toroli hawataweza kuvuka barabara kwa kutumia hayo madaraja kama ya manzese, labda wakati waupanuzi wa barabara tufikirie kujenga subways ambazo hata viwete na wasukuma toroli na guta watatumia kuvuka barabara. Tuangalie uwezekano wa Tanroad kushirikiana na sekta binafsi kujenga parking yards, mfano mtu anaweza egesha gari mbezi mwisho akapanda basi hadi kariakoo au posta, jioni akalipitia kwenda nyumbani.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment