Kumekuwepo na mgomo wa madaktari kwa siku kadhaa sasa ambao umeitishwa
na chama cha madaktari kuishinikiza serikali ili iweze kutekeleza
madai yao mbalimbali ambayo walikubaliana siku zilizopita .
Mgomo huu umeendelea hata baada ya serikali kusema kwamba baadhi ya
madai ya madaktari yameanza kutekelezwa na hata baada ya mahakama kuu
kutoa amri kwa mgomo huo kusitishwa mara moja ili wananchi waendelea
kupata huduma katika hospitali hizo .
Katika baadhi ya hospitali uongozi umeamua kusimamisha baadhi ya
madaktari na wasaidizi wao ili wale wanaopenda kufanya kazi wafanye
bila shinikizo lolote kutoka popote .
Kwa kuendeleza mgomo huu ina maana madaktari wanaenda kinyume na viapo
vyao walivyoapa , wanavunja mikataba yao ya kazi na wananyima wengine
haki zao za msingi za kuishi kama zilivyotamkwa katika azimio la umoja
wa mataifa kuhusu haki za binadamu ambalo Tanzania ni mwanachama .
Kwa kuwa madaktari wenyewe kupitia chama chao wameamua kuvunja
mikataba yao wenyewe na kuvunja haki za wengine kuendelea kuishi ni
vizuri sasa waambiwe basi inatosha , wasimamishwe kazi na washitakiwe
kwa makosa mengine dhidi ya binadamu .
Inasikitisha sana kuona daktari anagoma kwa ajili ya mshahara mdogo
huku mtu huyo huyo jioni anaonekana hosptali binafsi akitibu wagonjwa
wake , inasikitisha pia kuona mtu wa afya akilalamika upungufu wa
madawa huku akimwandikia mgonjwa dawa za kwenda kununua kwenye duka
lake nje ya hospitali .
Madaktari wa aina hii , madaktari maslahi hawatakiwi kuvumiliwa hata
wale watu haswa baadhi ya makundi ya wanaharakati , viongozi wa dini
na wanasiasa wanaoshabikia mgomo huu wa madaktari pia wapewe karipio .
Wanaharakati , viongozi , watu binafsi wanaoshabikia mgomo huu
wanauwezo wa kwenda hata nchi za nje kwa ajili ya matibabu kwa
kuchagua hospitali na hata wengine wapo huko huko kwahiyo haiwaumi
hata mgomo ukiwa wa maisha .
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment