Ni haki yao kabisa kujua idadi yao katika nchi,
Hakuna sababu ya msingi ya kuogopa hilo wakati linasaidia mengi
1) Kujua idadi ya watu kwa mgawanyiko wadini - Kwa kujua tu idadi halisi inasaidia kuliko kukisia kisia tu
2) kuna madai yaliyopo kwa waislam kuwa serikali inafungu ambalo inalipa Kanisa katoliki kila mwaka, ikifikia kuwa na wao wapewe then idadi ya waislam nimuhimu kujulikana hasa itapofikia kuwa fungu halitoshi kwahiyo labda ligawanywe
3) Elimu ni maneno tu yanasemwa saizi kuwa waislam wengi hawaja fikia elimu ya juu, tunatakiwa kujua idadi halisi na viwango vyao vya elimu
ukilinganisha na dini zingine, itasaidia kuwa serikali, taasisi za kiislam na jamii kuweka mkazo maeneo gani kwenye elimu
Hofu ya kuwa na mgawanyiko ni mawazo ya uoga tu, kipengele hicho kiingizwe ili zoezi likamilike, kinyume cha hapo fedha ya sensa itatumika nyingi na zoezo la sensa halijafanikiwa, litakuwa na haja gani. Kwa takwimu za UNHabitat wakristo ni asilimia 47% na waislam 48% kwa idadi ya watanzania wote. Ikiwa asilimia 48% ya watanzania wasiposhiriki, sensa inahaja gani???
Tunatakiwa kujua namba halisi kwa Wote Wakristo, Waislamu, Wa Bhudha, Bhahai, Wahindu, Wayahudi hata Wasio na dini. Wote wanaoishi nchini.
Hakuna dhambi kufanya hivyo, ingawa baadhi ya jumuiya za mashariki ya kati zinamaslahi ya kufahamu idadi halisi ya waislam tanzania, wengine wamejenga visima wilaya ya Ilala - Chanika, ambako concerntration ya waislam ni kubwa.
Na hata watu na taasisi zinazopata ufadhili toka OIC watahitaji kujua idadi ya waislam tanzania, just give them the (Number) kwa sbb hatakama hatuta wahesabu, bado wapo nawataendelea kuongezeka tu nchini.
From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, June 14, 2012 3:43 AM
Subject: [wanabidii] WAISLAMU KUGOMEA SENSA NI HATARI
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, June 14, 2012 3:43 AM
Subject: [wanabidii] WAISLAMU KUGOMEA SENSA NI HATARI
Ndugu zangu
Magazeti mengi ya leo yameandika kuhusu waislam wa Tanzania
kuhamasishana kugomea sense ya taifa inayotarajiwa kufanyika mwaka
huu .
Suala hili limenishangaza kama sio kunikatisha tamaa na harakati
kadhaa zinazofanywa nchini kwa misingi ya dini , ndio maana huko nyuma
niliwahi kukemea tabia za viongozi wa dini kujiondoa kwenye masuala
nyeti ya taifa kama haya ambayo yanaweza kuleta migogoro siku zijazo .
Suala la sensa sio la waislamu pekee ni la wananchi wote bila kujali
imani zao wala rangi , kabila na ukanda anao toka , ni kwa maslahi ya
taifa na watu wake ili kuweza kupanga mambo muhimu ya kimaendeleo kwa
sasa na kwa kizazi kijacho .
Suala la migomo dhidi ya masuala ya kitaifa limewahi kuwatokea puani
waislamu wa jimbo la kano nchini naijeria baada ya kugomea sense
wakati Fulani , kilichotokea kinajulikana na hata sasa hivi jimbo hilo
limeendelea kusumbuliwa .
Serikali ichukulie hatua viongozi wote wa kiislamu wanaopinga sensa na
wale wote wanaoendesha kampeni ya kupinga sensa ya watu ,walimu
mashuleni na sehemu nyingine za kukusanyikia watoto na makazini watu
wahimizwe kushiriki sensa .
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment