Thursday, 14 June 2012

[wanabidii] WAISLAMU KUGOMEA SENSA NI HATARI

Ndugu zangu

Magazeti mengi ya leo yameandika kuhusu waislam wa Tanzania
kuhamasishana kugomea sense ya taifa inayotarajiwa kufanyika mwaka
huu .

Suala hili limenishangaza kama sio kunikatisha tamaa na harakati
kadhaa zinazofanywa nchini kwa misingi ya dini , ndio maana huko nyuma
niliwahi kukemea tabia za viongozi wa dini kujiondoa kwenye masuala
nyeti ya taifa kama haya ambayo yanaweza kuleta migogoro siku zijazo .

Suala la sensa sio la waislamu pekee ni la wananchi wote bila kujali
imani zao wala rangi , kabila na ukanda anao toka , ni kwa maslahi ya
taifa na watu wake ili kuweza kupanga mambo muhimu ya kimaendeleo kwa
sasa na kwa kizazi kijacho .

Suala la migomo dhidi ya masuala ya kitaifa limewahi kuwatokea puani
waislamu wa jimbo la kano nchini naijeria baada ya kugomea sense
wakati Fulani , kilichotokea kinajulikana na hata sasa hivi jimbo hilo
limeendelea kusumbuliwa .

Serikali ichukulie hatua viongozi wote wa kiislamu wanaopinga sensa na
wale wote wanaoendesha kampeni ya kupinga sensa ya watu ,walimu
mashuleni na sehemu nyingine za kukusanyikia watoto na makazini watu
wahimizwe kushiriki sensa .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment