Siku chache zilizopita Taifa letu la Tanzania limepitiwa na upepo
mbaya wa kisiasa, sio mbaya sana ukilinganisha na upepo uliozipitia
nchi za Misri, Libya ,Tunisia na baadhi ya nchi nyingine za kiarabu
mwishoni mwa mwaka jana, lakini kwa utulivu wa kisiasa tuliokuwa nao
kwa miaka ya karibuni naweza kusema tumetikiswa kidogo na upepo huo,
hasa pale ilipofikia hata baadhi ya wabunge wa chama tawala
walipoingiwa na moyo wa uzalendo na kuweka sahihi zao katika orodha ya
wabunge waliokuwa tayari kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri
mkuu .Lakini kama kawaida chama cha mapinduzi ni chama kikongwe na
kiliutuliza upepo ule na waziri mkuu akapona.
Lingine lililotokea ni uteuzi wa wakuu wa wilaya mbalimbali ambapo
wakuu wa wilaya wapya 70 waliteuliwa kuongoza wilaya mbalimbali hapa
nchini.Baada ya uteuzi wa mawaziri na wakuu wapya wa wilaya kila mmoja
wetu alikuwa na maoni yake, ingawa wengine hawakupata fulsa ya
kuyafanya mawazo yao yasikike na watanzania wengi, lakini itoshe tu
kusema kwamba kila mtu alikuwa na wazo lake.Katika pitapita zangu
mitaani nilisikia na ninaendelea kusikia lawama kuwa Raisi
anapendelea, raisi anatoa fadhila kwa wanamtandao na hata kuna baadhi
walidiliki kusema kuwa raisi alisaidiana na mwanaye Ridhiwani kuteua
wakuu wa wilaya.
Ninachojiuliza zaidi na nashindwa kupata jibu ni je! Raisi amteue nani
ili amridhishe kila mtanzania?
Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amepewa mamlaka makubwa na
yasiyohojika kuteuwa viongozi mbalimbali , raisi anateua mawaziri na
manaibu wao wote, makatibu wakuu wa wizara wote, wakuu wa mikoa wote,
wakurugenzi wa halmashauri zote,wakuu wa wilaya zote
tanzania,majaji,wakurugenzi wa mashirika ya umma, mabalozi ,wakuu wa
vyombo vya usalama,wakuu wa vyuo vya umma vyote n.k. , hivi kwa mtu
aliyerundikiwa mamlaka ya kuteua watu wote hao ni kwa jinsi gani
anaweza akafanya uteuzi na akawaridhisha watanzania wote? mimi naamini
labda awe na uwezo wa malaika ndipo anaweza akawaridhisha watanzania
wote.
Hata angekuwa mtu mwingine yeyote lazima angemwita mtu wake wa karibu
ili amsaidie baadhi ya majina ili ayateuwe,(kama ni kweli mwanaye
Ridhiwani alihusika katika uteuzi).
Nini kifanyike? Ili kuondoa lawama zote hizi baada ya uteuzi wowote
ule kufanywa na kiongozi wa juu wa nchi Watanzania tutumie vizuri
fursa tuliyonayo mbele yetu ya kutunga katiba mpya, katiba
itakayompunguzia mamlaka mbalimbali mkuu wa nchi likiwemo na hili la
kupewa mamlaka ya kuteuwa viongozi mbalimbali kushika nafasi
nilizoziainisha mwanzo, tumpe mamlaka ya kupendekeza na bunge lipewe
mamlaka ya kupitisha au kukataa uteuzi.
vinginevyo hatutakiwa kumlaumu kiongozi ajaye maana fursa itakuwa
imeshapita na yeye hatakuwa na kosa kwa sababu katiba imempa mamlaka.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment