Katika siku za karibuni tumekuwa na kesi nyingi za wapenzi kuibiana
fedha , nyaraka na siri nyingine kwa njia ya mtandao haswa simu ,
barua pepe na mifumo mengine mbalimbali ya mawasiliano .
Kitu kilichogunduliwa baada ya uchunguzi mwingi ni kwamba wapenzi
wengi wanaaminiana sana haswa wanawake kuamini sana wapenzi wao wa
kiume kiasi kwamba atampa password za email yake , kadi yake ya benki
na hata siri za kazini kwake kisa anaogopa kuachwa .
Tukumbuke kwamba password au neno la siri ni mali ya mtu binafsi na ni
yako wewe mwenyewe , ukienda benki ukapewa password au neno la siri
kwa ajili ya kadi yako ya benki ni wewe umeingia mkataba na benki sio
mpenzi wako , mdogo wako au mumeo au jirani yako .
Sikatazi watu kupeana namba za siri manake kupeana muda mwingine
unajenga kuaminiana zaidi , kupendana zaidi na hata kuweza kusaidiana
katika mikasa ya hapa na pale endapo mtu ana hizo namba za siri huu
ndio uzuri wa kupeana namba za siri .
Ubaya wake ni mwingi na unaweza kuwa mchungu zaidi katika maisha yako
yote , kwa mfano mtu akakuta picha zako au nyaraka nyingine za siri
kwenye email zako akaamua kuzihifadhi sehemu nyingine kwa kuzichukuwa
baadaye ukaona picha hizo kwenye magazeti , blogu na sehemu nyingine
za kijamii , kwa nyaraka au namba za siri za benki mtu anaweza
kuchukuwa na yeye mwenyewe akaenda kukuibia hela au anaweza kumtumia
mtu mwingine ndani ya benki au nje kwa ajili ya kuhamisha fedha haswa
kiasi kikubwa cha fedha na usimwone tena pengine haswa kama mmeokotana
njiani .
Kama wewe ni muajiriwa na ukampa mpenzi wako password ya anuani pepe
yako akafanikiwa kuangalia mawasiliano yako na wafanyakazi ,
wasimamizi wako au hata siri nyingine za unapofanyia kazi hizi
zinaweza kuibiwa na kutumika dhidi yako au dhidi ya kampuni yako au
serikali yako muda wowote .
Hizo zote ni tisa kumi ni pale mpenzi wako anapoingia ndani ya barua
pepe yako na kuweka taarifa nyingine bila ya wewe kujua ili aweze
kuzitumia pindi mtakapoachana au kukorofichana , kwenye barua pepe
yako kuna sehemu inaitwa PASSWORD RECOVERY hata kwenye simu kuna
baadhi zenye huduma za Recovery .
Ukiwa kwenye barua pepe kuna kitu kinaitwa recovery Options hii
inayoweza kutumika ni kwa kuweka anuani nyingine ya barua pepe kwa
ajili ya kurejesha pwd kama imepotea au imesahaulika , saa nyingine
unaweza kutumia namba za simu kwa ajili ya kuweza kurudisha password
yako .
Unapomwachia mpenzi wako password yako anaweza kuingia kwenye barua
pepe yako na kubadilisha hizo taarifa pale kwenye recovery email
ataweka yake unayoijua au usiyoijua , kwenye namba za simu anaweza pia
kuweka zake . ikiwa ndio hivi ataweza kubadilisha password muda wowote
akitaka na wewe usiweze tena kuingia katika anuani hizo .
Nakumbusha tena kwa kuuliza unamwamini mpenzi wako na password ? kama
unamwamini hongera zako lakini ujue password ni mali binafsi na anuani
pepe ni mali binafsi pia labda kama kuna makubaliano mengine ya
ziada .
NB : Hii haihusiani na pale unapotegeshewa programu ya kunukuu na
kuhifadhi password kwenye ma internetcafe au maofisini zinazoitwa
KEYGEN . Keygen ni mada tofauti ingawa ukishtuka password yako
imeibiwa unauwezo wa kubadili password haraka .
USHAURI WANGU
Hakikisha unabadili password zako za barua pepe , kadi za benki , simu
na vifaa vingine mara kwa mara na hakikisha taarifa hizo zinatunzwa na
kama unashare na mtu hakikisha unakuwa na njia mbadala za kuweza
kurecover namba za siri kama zimepotea mara moja la sivyo siku utakuja
lia .
YONA FARES MARO
0786 806028
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment