Friday, 29 June 2012

[wanabidii] TUOGOPE MAGARI TINTED!

This was forwarded to me, tuisome!
 
Dear friends Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa
mfanyakazi mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki
iliyopita. Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa
siku hiyo ya tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea
viwanja vya biafra. Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa
hiyo aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja.
 
 Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx amepata ajali na kufa
papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili hospital. Baada ya
kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu. Tulijaribu kuipiga
iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita
bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, ma
baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia
maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier
wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na taarifa
zake.
 
Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya
usalama barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za
ajali mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa
taarifa polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata.
Wakati huo huo ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja
wakiendelea na jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku.
 
Kilichokuwa kinatia wasiwasi zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba takribani
zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake hawakuwahi kuona
ndugu yao akichelewa kiasi hicho.
 
Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango, alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa
na uwezo wa kuzungumza sana, ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada
ya muda hospitali ya mwananyamala. Alipopata nguvu alianza kuwasimulia
nduguze kilichotokea. Alipotoka ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye
kituo cha daladala cha karakana, pale kituoni walikuwa abiria wawili
yaani yeye na mama mmoja. Baada ya dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa
mbele Kawe na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu
alikuwa anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili
wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver. Gari hiyo
hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu
moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na
walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na
kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi
pia ana miaka 32.
 
Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na
walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka
akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa
kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu.
 
Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa
nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa
cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya
muda akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno lamwisho analokumbuka
alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize kazi. Kilichomwamsha
ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na
kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga.
Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa
dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na
walikuwa wamevaa gloves.
 
Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu
kingine.  Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali wanachokitumia, na
walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa lazma ziwe za mtu
wa miaka 40 na kuendelea. Mwenzao mmoja akasema cashier alisema alikuwa
na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake inaonyesha kazaliwa
mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila
waliendelea kumkung'uta kwa hasira. Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo
iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya
sayansi.
 
Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote,siku
iliyofuata alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea
vzr. Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia
abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata
vyeo na utajiri wa haraka Sent from my BlackBerry® smartphone provided
by Airtel Tanzania. -- 'Friends, Social Economic Association (FSEA),
Together we move forward!'. -- 'Friends, Social Economic Association
(FSEA), Together we move forward!'. -- 'Friends, Social Economic
Association (FSEA), Together we move forward!'. -- - Kilimo kwa Maendeleo
yetu na Taifa -_______________________________________________
UDASA mailing list
UDASA@udsm.ac.tz

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment