Friday, 29 June 2012

[wanabidii] TAARIFA JUU YA USAJILI WA MELI ZA NJE ULIOFANYWA NA SMZ

TAARIFA KWA BARAZA LA WAWAKILISHI JUU YA
USAJILI WA MELI ZA NJE ULIOFANYWA NA SMZ
KUPITIA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI
ZANZIBAR MARITIME AUTHORITY – ZMA
Friday, June 29, 2012

Mhe. Spika,
Tarehe 27/06/2012 Vyombo vya Habari hapa Tanzania (The Citizen) na
nchi za nje (International news Agency – Bloomberg) viliandika makala
kuhusu usajili wa meli 10 za mafuta (Tankers). Ilidaiwa katika makala
hayo kuwa Meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya
Tanzania na kwamba zinafanya biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN.
Gazeti la "The Citizen la tarehe 27 Juni, 2012 lilikuwa na kichwa cha
habari "Iran Tankers adopt TZ Flag to avoid embargo" (meli za mafuta
za Iran zinatumia bendera ya Tz kukwepa vikwazo.

TAARIFA YA ZMA

Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar Maritime Authority – ZMA ni
Mamlaka iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na
kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari
Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).

Sheria ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006, kifungu no. 8 cha
sheria hii, kinasomeka kama ifuatavyo:

Section 8 (1). There shall be established the registers of Tanzania
Zanzibar ships to be Known as:-

o (a). Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean
going ships; and

o (b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships.

• (2). A ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for the purpose of
this Act if that ship is registered under this part.

Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika
kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana
mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za
kimataifa. (Open Registry). Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka
2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni
pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.

Kama nilivyoeleza hapo awali, vyombo vya habari vimechapisha makala ya
usajili wa meli 10 ambazo zinadaiwa ni meli za IRAN kulingana na
makala zao hizo.

SMZ inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta ilizosajiliwa wiki
mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya
makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata
usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:

Jina la meli GRT (Ukubwa) Company name Ilikotoka

1. Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta

2. Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus

3. Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta

4. Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta

5. Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus

6. Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta

7. Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta

8. Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta

9. Courage 163660 Courage Shipping Co. ltd Cyprus

10. Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus

11. valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus

Jumla ya GRT ni 1,388,368 tons

Meli hizi ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni
mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration). Meli
zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta. Sambamaba na
meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo
zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha
usajili wao na kwenda usajili wa "TUVALU Islands".

ZMA ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizi
na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni
ya mafuta ya IRAN. Philtex ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis
tarehe 28/06/2012 katika afisi za Philtex Corporation na Wamiliki hao
wameeleza kwamba hawana uhusianao na Serikali au mamlaka yoyote nchini
Iran na wameamua kuja kusajili meli ZMA kwa ridhaa yao na kwa kufata
matangazo ya usajili wetu wa nje (Open Registry).

Pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza kwamba ikiwa ZMA
haiko tayari kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta usajili
wao na tayari wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine
(PANAMA) lakini hawana nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na
Malta.

Kinyume na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari juu ya uraia wa
wamiliki wa meli hizi, Wamiliki wa meli hizi kama walivyojieleza
katika usajili wa meli zao wana uraia wa British Vergin Islands na
Sychelles.

Kulingana na "United Nations Convention Law of the Sea", Article 91,
na za "Geneva convection of Registration" articles 6, 7 na 8, na
kulingana na Zanzibar Maritime Transport Act of 2006, section 8,
Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili meli yeyote kulingana na
taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa zinazoongoza
usajili huo.

Maelezo haya yanatolewa ili kutoa usahihi wa uvumi kuwa Zanzibar
imesajili meli za IRAN ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na nchi
za Umoja wa Ulaya (European Union) juu ya usafirishaji na uuzaji wa
mafuta kutoka Iran.

Mhe. Spika, taarifa hizi za vyombo vya habari hazina madhumuni yeyote
zaidi ya kuwavunja moyo wenye Makampuni ya meli wanaotaka kusajili
meli zao kwetu.

Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli
hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali
imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli
mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya
nchi. Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha
wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa
zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine
zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na
uchumi wake.

Hata hivyo mamlaka itafata sheria zote zilizowekwa kitaifa na
kimataifa katika biashara ya usafiri baharini na itahakikisha meli
zinasajiliwa chini ya mamlaka hii zinafata taratibu ilizoweka.

Mhe. Spika, kabla ya taarifa hizi za vyombo vya habari (The Citizen),
Waziri wa Uchukuzi wa SMT Mhe. Harisson Mwakyembe) alipokuwa akijibu
suala Bungeni hivi juzi hakuonyesha kurishika kwake katika usajili wa
meli (Open Registry) inayofanywa na Zanzibar na kuahidi kufanya ziara
ya kuja Zanzibar kuonana na Waziri anaehusika kuzungumzia suala hili.
Taarifa za "The Citizen" zaweza kuwa ni muendelezo wa Mhe. Mwakyembe
kutoridhika kwake katika usajili unaofanywa na Serikali kupitia
uwakala wake huko Dubai.

Mhe. Spika, Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi yeyote.

Hili ni suala la kibiashara na kwamba kwa Serikali yetu ni njia moja
ya kuongeza mapato yanayoendesha Serikali, alimradi tu usajili huo
hauvunji sheria za Kimataifa.

Mhe. Spika,

Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo
IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran)
na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani IRAN itaendelea
kusaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo. Zanzibar haingependa
kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro
isiyowahusu.

Hivyo, kwa taarifa hii, Serikali inakanusha rasmi uvumi wa vyombo vya
habari kuhusiana na suala hili kama taarifa hii ilivyofafanua hapo
juu.

Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.

Hamad Masoud Hamad

WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO

Chanzo: Zanzinews

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment