HABARI ZA MAPAMBANO NDUGU ZANGU WANABIDII
MAMBO MENGI YAMESEMWA KUHUSU BUNGE LA SASA, NA MIMI NAOMBA NISEME KIDOGO YA KWAMBA KINACHOTOKEA HIVI SASA BUNGENI HAKUNA WA MTU YOYOTE WA KUKIZIMA, SIO CCM WALA SIO UPINZANI HAKUNA WA KUKIZIMA HATA KIDOGO.
NASEMA HIVYO KWA SABABU KIZAZI CHA KUOGOPA NA KULINDANA KINAELEKEA MWISHO NA KIZAZI KILICHOPO SASA NI KILE KISICHOOGOPA KUSEMA KILE KINACHOAAMINI KUSEMA NA WALA HAKIHOFII CHOCHOTE KATIKA MAISHA.
SIKU ZA NYUMA BAADHI YA MAKADA WA CCM WALIKUWA WANAFIKI NA KUHOFU AMBAPO WALIJIKUTA WAKIFUATA MKUMBO KATIKA MAMBO FULANI FULANI KUTOKANA NA KUOGOPA KUPOTEZA NAFASI ZAO WALIZONAZO KISIASA..
VIJANA WAKIWEMO WABUNGE VIJANA MIMI NAAMINI WAMEDHAMIRIA KULETA MABADILIKO KATIKA JAMII, LAKINI PIA KUNA BAADHI YA WATU WANADHANI WAWAKILISHI HAO WANAFANYA MAIGIZO HUKO BUNGENI.
"KUNA MSEMO USEMAO KWAMBA, MTU AKIWA NA JAMBO LA KUSEMA KWA ANIABA YA JAMII ENDAPO ATAKAA KIMYA BASI MAWE YATASEMA BADALA YAKE, WABUNGE VIJANA MUUNGANE NA KUISEMA SERIKALI MUDA WOWOTE MNAPOPATA NAFASI HIYO NA NAAMINI KUNA SIKU JAMII ITAWAELEWA.
MKINYAMAZA MAWE YATASEMA, MKIKAA KIMYA 2015 SIO MBALI MTAKUTANA NA WAPIGA KURA WENU NA WATAWAULIZA MBONA TULIWATUMA KWENDA KUTUSEMEA BUNGENI MBONA MLIKAA KIMYA?
WANABIDII PAMOJA NA SHUGHULI ZETU KUWA NYINGI NAOMBA TUPITIE PALE DODOMA TUWATIE MOYO HAWA WABUNGE VIJANA ILI KUWAWEZESHA WANANCHI KUSEMEWA MATATIZO YAO.
NASEMA VIJANA KWA SABABU HAWA WAZEE WAO HAWANA JIPYA NA MBUNGE KIJANA AKIONEKANA ANAZUNGUMZA WANAMUONA NA MLETA VURUGU LAKINI BAHATI MBAYA HAWAFAFANUI NI VURUGU GANI ANAZOFANYA
PIGA VITA NENO NAUNGA MKONO HOJA YA SERIKALI MIA KWA MIA
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment