www.knbs.org.ke/census,
www.ubos.org,
www.abs.org.au.census
www.12.statcan.ca/census
www.ons.gov.uk/census
Kwenye tovuti zote hizo unaweza kupata habari juu ya sensa za makazi
na watu kwa nchi za wenzetu wanafanya sensa ikiwa na kipengele cha
dini kikiwepo. Watu watakuwa na rejea ya uhakika. Hata kama watu
wengine watatoa taarifa zao taarifa za kuaminika zitatoka ktk ofisi ya
serikali , hakutakuwa na ubabaishaji kama ilivyo sasa ambapo unaweza
kua malalamiko zaidi hatimaye kuvunjika kwa amani.
Mfano unaotolewa na Serikali kuhusu Nigeria haujazingatia nchi
nyingine ambazo zinafanya sensa hizi kwa Mafanikio kama UK, Australia,
Canada, Uganda, nk
Ni Marekani tu ndio iliyoa kipengele hiki kwa sababu zake binafsi.
Wanaotawala wachache hawataki wajulikane kuwa ni wachache.
Msimamo wa Waislam juu ya Sensa ya August 2012
1.Kipengele cha dini kiwepo ili kuondoa utata uliopo sasa kwa kupata
taarifa rasmi za kiserikali kuliko kuacha kila mtu atoe za kwake, hali
hii inaweza kuchochea kuvunjika kwa amani
2. Iundwe tume huru kusimamia zoezi la kuhesabu watu ili kila kundi
liridhike
3. Serikali itunge sheria na kuisimamia kupiga marufuku utoji takwimu
holela hasa katika shughulirasmi na za serikali jambo ambalo linaweza
kuleta uvunjifu wa amani na utulivu kama walivyofanya TBC1 kwa kurusha
taarifa zisizorasmi za sensa.
Kuendelea kupuuza malalamiko haya ni kukaribisha hisia za dharau, na
kutosikilizwa kwa waislam ambako knaweza kuleta shida siku za usoni.
Tamko hili limesomwa na Sheikh Musa Kundecha kwa niaba ya Sheikh
Mohamed Mtuliya (BAKWATA) ambaye ni Mwenyekiti wa Viongozi waliotoa
Tamko.Viongozi hao ni wawakilishi wa Taasisi kubwa za kiislam
zifuatazo;
1. BAKWATA
2. BARAZA KUU
3. SHIA ITHNAASHERI
4. JOPO LA MAULAMAA TANZANIA
5. HAIYATUL ULAMAA
6. JUMUIYA YA BOHORA
7. UMOJA WA WAHADHIRI TANZANIA
8. JUMUIYA YA WATAALAM WAISLAM TANZANIA
9. SUNNI JAMAAT
10.JUMUIYA YA ISMAILIYA TANZANIA
Chanzo: Michuzi Blog
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment