"Afadhari vita inayo saka haki na heshima kuliko amani inayo pumbaza
akili na kudhalilisha utu wa mwanadamu" haya ni maneno yanayo penda
kutamkwa na aliyekuwa Mheshimiwa mbunge wa Arusha mjini kila alipopata
fursa ya kuongea na wananchi, mara ya mwisho nimemsikia akitamka
maneno hayo kwenye uzinduzi wa M4C tarehe 26 Mei 2012.
Mtakumbuka kuwa alinyang'anywa ubunge kwa hukumu ya mahakama. Hukumu
ambayo ilizaa minong'ono na kupigiwa kelele kwenye kila kona ya
wapenda haki. Na hata alipo kuwa anahutubia umati wa wanachama wa
Chadema pale NMC mwenyeki wa Chadema mheshimiwa Mbowe alisema
"Hatuwezi kunyamaza kwa kukubali hukumu yenye maamuzi ya kihuni na
ukandamizaji wa haki" ukumbuke pia kuwa kauli ya Mbowe ilisha
tanguliwa na kauli ya Godbless Lema mara tu baada ya hukumu iliyo
mpoka ubunge wake, alisema "Nilishapata taarifa mapema juu ya
hitimisho ya kesi hii, nimenyang'anya ubunge kwa maelekezo ya mkubwa
wa ikulu".
Kama mtakumbuka siku hiyohiyo kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ikatoa
tamko (taarifa kwa vyombo vya habari) kukanusha kauli za Lema. Kwenye
taarifa hiyo kwa vyombo vya habari yalitumika maneno na kauli zilizo
zaa mijadala mipya mitaani kwa walala hoi hai. Moja ya wapo ya kauli
ilisema kwenye taarifa ile ilisema "Mheshimiwa lema aache kutapatapa
na asimtafute mchawi... Apuuzwe maana kauli zake ni upuuzi mtupu"
lakini pia taarifa ile ilisema "Rais hakufanya mawasiliano ya aina
yoyote iwe ya simu, au barua kuingilia uhuru wa mahakama"
Jana kwenye hotuba yake ya mwisho wa Mwezi wakati rais anahutubia alisema "
Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na
shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na
kuwakarimu vyema
wageni wetu
hao. Nawaomba
waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka
wote. Naomba
kuwepo kwa mkutano huu
kuwakumbushe umuhimu
wa mji wenu kuwa tulivu.
Miaka miwili iliyopita
isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki
hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe
hata sisi wenyewe
tusinge shawishika kuomba au kukubali maombi ya
namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila
mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la
kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima
iendelee kuangaza.
Yaliyopita si ndwele
tugange yajayo."
kwenye hiyo kauli hapo juu kuna kifuniko cha siri ambacho ni mkuu tu
peke yake ndio anajua kinafunguliwaje. Miaka miwili iliyopita Arusha
haikuwa na amani?! Nani aliitoesha amani iliyokuwa Arusha?! Wenye
dhamana ya kusimamia na kuidumisha amani nao walikuwa hawataki Arusha
iwe Geniva ya Afrika?! Kwani hiyo miaka miwili iliyopita, yaani baada
ya uchaguzi wa 2010 hadi mwaka huu 2012 nani alikuwa muwakilishi wa
wananchi aliye shindwa kuihubiri amani na kuiacha itoweke?! Yeye ndio
alitoesha amani na kuharibu sifa ya Geniva kwa kuwauwa raia 3 mmoja
akiwa wa nchi jirani?! Kwa nini yaliyopita yaitwe ndwele ili tusi
yagange hasa kwa Arusha? Na tusigange yapi, ya kutokuwa na amani
Arusha au zile lawama za kipuuzi za kuingilia uhuru wa mahakama? Au
tusiyagange kwa wananchi wa Giniva kutokuwa na muwakilishi wanae
mpenda hata kama anatafsirika kuwa anapenda kwenda jela pale anapo
tishiwa kuuwawa?
Mimi sio mbobezi wa somo la Mantiki (logic) bado ni mwanafunzi ninae
jitahidi kulifaulu somo hilo. Tunao magwiji wabobezi wanaojua tundu la
sindano linaingia uzi wenye ukubwa gani. Wanaweza kung'amua maneno
aliyo shona mkuu kwenye hotuba yake ikiwa ni pamoja na kuunganisha
nukta za kauli za mara kwa mara za yule mkuu wa mkoa wa Arusha.
Labda nitamuuliza lakini sijui kwa nini Lema hupenda kusema "Afadhari
vita inayosaka haki na heshima kuliko amani inayo pumbaza akili na
kudhalilisha utu wa mwanadamu"
Nimeamka angalau niandikea baada ya kukumbuka maneno ya Martin Luther
King alie kuwa mpigania haki za weusi kule Marekano. Alisema "Our
lives begin to end the day we become silent about things that matter",
halafu aliwahi kusema tena "It has come a time when silence become a
betrayal"
--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
+255 (0) 713 (784) 24 67 64.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment