HII NI BARUA YA JUMUIA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR.
Na Masoud Ali
Kwa ndugu waislamu na wote wapenda haki na wanaoipendelea maslahi mema
zanzibar.
Umoja wa Jumuiya na taasisi za kiislamu Zanzibar umeamua kuandika
barua hii ya wazi kwa ummma wa Wazanzibar, viongozi na wananchi
kutokana na tuhuma kadhaa zilizoelekezwa kwa jumuiya ya Uamsho.
Awali tunapenda ifahamike kuwa harakati za kuikomboa Zanzibar ili
ipate mamlaka yake kamili na kuirejeshea heshima yake ni harakati
zinazosimamiwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu si jumuiya ya Uamsho
peke yake kama wanavyojaribu kwa makusudi vyombo vya habari kupotosha
ukweli ili kudhoofisha harakati hizo za ukombozi kuipelekea Zanzibar
kupata mamlaka kamili (sovereign state).
Kumejitokeza maadui wengi wa harakati hizi kwa kuituhumu jumuiya hiyo
ina uhusiano na makundi yenye msimamo mkali wa kiislamu na wengineo
wamekua wakisema wazi kuwa Uamsho ina uhusiano na makundi ya Al-Qaeda,
Alshabab, Boko haramu na mengineyo. Uvumi mwengine ni kua jumuiya ya
Uamsho inashirikiana na Marekani katika kuendesha harakati zake, vile
vile ina uhusiano na chama cha Hizbu Tahrir na Chama Cha Wananchi –
CUF.
Tuhuma hizo zimetolewa na viongozi wa makanisa sambamba na viongozi wa
CCM kama NAPE pamoja Mh. ALI HASSAN MWINYI na wenziwe pamoja na watu
wanaoheshimika na wenye dhamana kubwa katika jamii na kwa hamasa kubwa
sana, hayo yametamkwa hadharani bila ya kuwa na ushahidi wowote.
Tuhuma hizo zimetolewa ili kuwapoteza malengo Wazanzibar na kuvuruga
umoja wao katika kudai haki zao za msingi ambazo ni kudai utaifa wa
nchi yao. Njama za kuvuruga umoja wa Zazanzibar hazikumalizia katika
tuhma tu bali hivi sasa zinaandaliwa nama za kughushi Account katika
mabenki ambazo zitaihusisha jumuiya ya Uamsho kuwa inapokea misaada
kutoka makundi ya Al-qaeda, Al-shabab na mengineyo na njama nyengine
ambazo hazijatajwa kwenye maelezo haya. Zaidi kuliko hayo viongozi wa
kanisa wameanza harakati za kuziburuza serikali zote mbili na kutumia
vyombo vya dola kwa lengo la kuvunja katiba na amani ya nchi kwa
kuzitaka serikali kuingilia uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni kwa
kuwanyima waislamu na kuwapiga marufuku haki yao ya kuabudu na uhuru
wa maoni kupitia mihadhara, dua, itikafu, nk. Ifahamike kwamba katiba
zote mbili zinalinda haki hiyo ibara ya 19. ya katiba ya Jamhuri ya
Muungano inasema (1,2) kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa
mawazo ,imani na uchaguzi katika mambo ya dini…..kazi ya kutangaza
dini kufanya ibada na kueneza dini ni huru na jambo la hiari….shughuli
na uendeshaji wa jumuiya za kidini zitaka nje ya shughuli za mamlaka
ya nchi.(rejea ibara ya 18,19,20 ya katiba ya zanzibar).
Hivyo umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu inapenda kuwataarifu
wananchi wa Zanzibar, wanaoipendelea mema Zanzibar na wapenda haki
kote duniani kuwa Jumuiya ya Uamsho haina uhusiano wowote na makundi
yaliyotajwa hapo juu kwani hakuna haja wala hoja ya kutaka misaada
yeyote kutoka kwao. Pia inasisitiza kuwa Junuiya ya Uamsho ni vuguvugu
la umma la Wazanzibar ambao hawajajiambatanisha na makundi yoyote
yenye kufanya mapambano na tawala zao kwa njia ya silaha, wala
haijajiambatanisha na nchi au taasisi yeyote ya nje ya nchi na ndani
kwani hakuna haja wala hoja ya kufanya hivyo.
Jumuiya ya Uamsho inafanya kazi hiyo kwa kushirikiana kikamilifu na
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu tofauti nchini Zanzibar kwa kutetea
maslahi ya kupatikana kwa mamlaka kamili ya Serikali ya Zanzibar
kutokana na kushindwa kwa vyama vya siasa kutetea utaifa wa Zanzibar
kwa sababu vyama vya kisiasa vimezingirwa na katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
Katika hali hiyo ni nani angejitolea kulizungumza jambo hilo? Chombo
pekee ambacho ndicho kinawakilisha umma wa Zanzibar ni Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu na kukabidhiwa jukumu la mambo tofauti. Jumuiya ya
Uamsho ambayo ndio yenye sauti pekee katika jamii na kwasababu hiyo
imelazimika kutoa sauti ambayo hakuna mwengine angeliweza kutoa.
Watu wa Zanzibar wajuwe kuwa wachache wasioipendelea mema Zanzibar
hawatasita kuunda kila njama za kuharibu vuguvugu la kudai mamlaka
kamili ya Zanzibar. Viongzi wa jumuiya wanawataka Wazanzibar watambue
njama hizo na wasiyumbishwe katika msimamo wao.
Jumuiya ya Uamsho si kundi la magaidi, wala si kundi la wachoma moto
makanisa au waporaji wa mali za umma. Jumuiya ya Uamsho inatoa sauti
kwa njia za amani bila ya kutumia nguvu za silaha bali kwa kutumia
nguvu za hoja na inaendesha harakati zake juu ya misingi ya sheria za
nchi na katiba.
Wananchi wa Zanzibar kudai uhuru wa kujiamulia mambo yetu ni haki yetu
ya msingi na kwa hilo HATUNA MJADALA MPAKA KIELEWEKE, tutaendelea
kudai haki zetu kwa kila hali bila ya kuvunja sheria za nchi.
Tunasisitiza kuendelea na kudai Zanzibar huru ingawa tunaelewa gharama
ya kufanya hivyo ni kubwa ikiwemo kupoteza roho zetu kwa mfano aliekua
Rais wetu wa kwanza Almarhum Abeid Aman Karume alipoteza uhai wake
baada ya kuanza kuugusa muungano pale alipopiga marufuku azimio la
Arusha kutumika Zanzibar na kusema mwisho wake Chumbe pia na kusema
muungano ni kama koti likikubana unalivua haukupita muda alipoteza
uhai wake.
Mzee wetu mheshimiwa Aboud Jumbe alipotengeneza mazingira ya muungano
wa haki alikwenda Dodoma akiwa RAIS alirudi akiwa raia wa kawaida
aliuzuliwa urais. Hayo ndio matokeo ya kuugusa muungano. Watu
walipoteza mali zao, heshima zao na roho zao eti kwa sababu ya kuugusa
muungano.
Wazanzibar tutaendelea kudai Zanzibar yetu huru. Kama sheria
zinavyoelekeza ikiwemo kudai kuwepo kwa KURA YA MAONI kwa njia ya
amani.
TUWACHENI TUPUMUE!!!!!!!
WABILLAHI TAUFIQ….
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment