Tarehe 5 Juni,2012, mfanyakazi waKampuni ya Magazeti ya Serikali
(TSN), ambaye amelemaa baada ya kupata ajali yagari, Bwana Athumani
Hamisi, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenyeukumbi wa
Maelezo, Dar es Salaam, na kutoa taarifa iliyojenga taswira
kuwaametelekezwa na TSN pamoja na Serikali.
TSN inapenda kufafanua kuwa Serikalina kampuni hii, ambayo ilimwajiri
Athumani tarehe 1/09/2006 kama Mpiga pichaMwandamizi, wamemhudumia
mfanyakazi huyo kikamilifu tangu alipopata ajalitarehe 12 Septemba,
2008 hadi sasa, na huduma hiyo inaendelea.
Baada ya kutokea ajali hiyo, TSN kama mwajiri ilisimamia matibabu yake
ya awali katikahospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa
(MOI) mpaka Serikali, kwakupitia Wizara ya Afya ilipomhamishia
Netcare Rehabilitation Hospital nchini AfrikaKusini kwa matibabu
zaidi.
Serikali ililipia gharama za matibabuyake yote akiwa Afrika Kusini kwa
kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba, ambayoyanazidi shilingi milioni
mia moja.Gharama hizo ni pamoja na ununuzi wa kigari maalum ambacho
Athumani anatumiasasa.
TSN kama mwajiri ililipa nauli yandege kwenda na kurudi pamoja na
posho ya kujikimu ya mgonjwa pamoja na nduguwasindikizaji ambao ni Bw.
Hassan Hussein na Bi. Mirriam Malaquias.Posho yakujikimu ilikuwa USD
6,210 sawa na Shilingi 9,315,000, na nauli kwa watu watatu ilikuwa ni
Shilingi3,535,869.92. Athumani aliendelea kupatiwa huduma akiwa huko
Afrika Kusini kwagharama za Serikali na TSN mpaka aliporejea nchini
tarehe 08/05/2010. Gharamazilizolipwa na kampuni kwa mfanyakazi huyu
hadi sasa ni takriban shilingi million 52.
Athumani aliporejea nchini alilakiwana wafanyakazi na viongozi wa TSN
na kupangiwa chumba hoteli ya Holiday Inn wakatiutaratibu wa
kumtafutia nyumba ya kupanga ukikamilishwa. Kampuni ilitumia kiasicha
Shilingi 1,756,979.50 kulipia hoteli. Baadaye alipelekwa kwenye
nyumbaambayo alipangiwa na Kampuni katika eneo la Sinza Vatican ambapo
ndipo badoanaishi hadi hivi sasa. Gharama ya nyumba kwa mwaka wa
kwanza 2010 ilikuwa niShilingi 4,200,000 au Shilingi 350,000 kwa
mwezi. Mwaka 201 mwenye nyumba alipandisha kodi hadi400,000 kwa mwezi
ambapo Kampuni ililipia Shilingi 4,800,000. Kodi hiyoimeishia Mei
mwaka huu na kampuni imeshafanya mazungumzo na mwenye nyumba
iliAthumani aendelee kuishi hapo kwa muda wakati mipango endelevu ya
ustawi wakeinafanywa kwa kuzingatia taratibu za ajira.
Mnamo tarehe 8/12/2010 Athumanialirudi tena Afrika Kusini kwa ajili ya
uchunguzi wa maendeleo ya afya yake namatibabu yaligharimiwa na
Serikali wakati TSN iligharamia nauli yake na yamuuguzi wake, pamoja
na posho ya kujikimu Shilingi 6,300,000/-.
Pamoja na bwana Athumumai kulalakitandani kwa muda wote huo ameendelea
kulipwa mshahara kamili bila kukatwakama mfanyakazi wa kawaida ikiwa
ni msaada wa kampuni kwa kuzingatia ulemavualioupata.Mshahara
aliolipwa kwa muda wote aliokuwa anaugua ni kiasi chashilingi
26,773,000. Vile vile kampuni ilimlipa muuguzi toka Afrika
Kusiniambaye alikuwa anamhudumiaa Athumani Rand 12,500 kama mshahara
wake.
Kuanzia Januari 2011, mshahara waAthumani umejumuisha asilimia 15 kama
posho ya nyumba ambayo wafanyakazi wotewanalipwa. Aidha Athumani yupo
kwenyempango wa bima ya afya anayolipiwa na kampuni, ambayo
inamwezesha yeye nafamilia yake kuweza kutibiwa katika hospitali
yoyote hapa Tanzania. Kampuni inamlipia Shilingi 68,449.20 kilamwezi
na bima hiyo ndiyo inayogharamia matibabu yake yote hapa nchini.
Bwana Athumani anapatiwa usafiri naTSN mara mbili kwa wiki kumtoa
nyumbani hadi Muhimbili na kurudi kwa ajili yamazoezi ya viungo.
Imetolewa na
OFISI YA MHARIRI MTENDAJI
08.6.2012
------
*Chini ni Nakala ya Maombi ya Mpiganaji Athumani Hamisi Aliyoitoa Kwa
Waandishi Wa Habari Jijini Dar es Salaam Juzi
---
Mimi Athumani Hamisi
Awali ya yote, napenda kuwasalimia wote, wakubwa na vijana wenzangu
Hii itakuwa mara ya pili kuongea nanyi waandishi wenzangu, ndani ya
miaka minne tokea nipate ajali Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani
Pwani nikiwa na wenzangu Herry Makange ambaye kwa sasa ni marehemu na
Anthony Siyame, tukiwa njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi kikazi. Mara
ya kwanza niliongea nanyi 2010 baada ya kurejea kutoka Afrika kusini
nilikopelekwa na Serikali kwa matibabu.
Shukrani zangu za awali, zimwendee Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Kikwete aliyenitembelea katika Hospitali ya Muhimbili
nilikolazwa na kuagiza nilipelekwe nje kwa matibabu zaidi.
Katika ajali ile, nilivunjika shingo na ku-damage spinal cord
iliyopelekea kupooza mwili wote kuanzia shingoni. Katika operesheni
iliyofanywa na madaktari wa hospitali ya Mil Park, Afrika Kusini
walilazimika kuunganisha shingo kwa nyuma.
Shukrani za pili ni kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni
ninayofanyia kazi ya magazeti ya serikali, wachapishaji wa Daily News,
Sunday news, Habari Leo Jumapili na Spoti leo, familia yangu iliyokuwa
katika wakati mgumu wakati huo hadi sasa watanzania wote wuamini wa
dini zote waliokuwa wakiombea Pamoja na marafiki zangu waliokuwa
wakihangaika huku na kule kwa namna moja ama nyingine .
Niko mbele yenu leo kuwaomba mnifikishie ujumbe kwa jamii kwa maelezo
yafuatayo:-
Ofisi yangu ya TSN ilinipangia nyumba ninayokaa Sinza Vatican,
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mei 2010-2011 na mkataba
ulikukwa kati ya mwenye nyumba na TSN ambao mimi sikuwahi kuuona hadi
ninavyoongea na nyie leo.
Mkataba uliisha tena Mei 2011, mwenye nyumba alikwenda TSN kuomba
kusaini mkataba mpya. Badala yake aliandikiwa mkataba mpya wenye jina
langu na kupewa aniletee mimi nisaini. Nilipomuuliza mkataba wa kwanza
uliingia na nani na ni nani alisaini. Alisema ni TSN walisaini
wakamwambia wana mgonjwa ambaye ni Staff wake atakuja kuishi pale
akitokea Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu. Mwenye nyumba akasema
walimwambia gharama za nyumba ni za TSN , sasa nashangaa leo
wameandika jina lako na mkataba ni kati yangu na wewe.
Nikamwambia kaka, mimi sikutarajia kufikia hapa kwani mwaka 1999
ilipangwa mimi nifikie katika nyumba ya kampuni Upanga kuepusha
gharama na ukaribu wa huduma za kitabibu, mpaka masuala yangu
yatakapothibitishwa na Daktrari kama hali yangu itaruhusu mimi kuweza
kufanyakazi ama vinginevyo. Rudi ofisini mkasaini kama mlivyofanya
awali. Na umwambie kwa hali ya Athumani hawezi kusaini mkataba na mimi
kulingana na hali yake. Isitoshe mi nilitiliana saini mkataba wa awali
na TSN.
Ukweli nilikataa kusaini zaidi ya mara tatu, mpaka Meneja Mwajiri
siyo huyo wa sasa alipoingilia kati na kunithibitishia kuwa kampuni
italipa nyumba mpaka uamuzi wa madaktari utakapotoka, saini mimi
nitakulinda. Niliporejea nyumbani nikawekwa wino katika dole gumba
wakaweka saini. Mpaka yalipojitokeza ya sasa.
Ndugu waandishi wa habari, hali yangu japo imeimarika zaidi kuliko
awali, leo nimekuja na jambo ambalo litahusisha jamii na nyie ndiye
wahusika wakuu katika suala hili.
KIKUBWA ZAIDI LEO NI SHUKRANI NA OMBI
Ukweli ulio wazi, nashukuru kwa Mungu na kujivunia kuwa TSN .
nimelelewa na TSN kwa miaka sita sasa. Imenilea nikiwa mgonjwa kwa
miaka mine, nikiwa bado niko ndani ya ajira jambo ambalo ni gumu sana
sehemu nyingine.
Imelipa nyumba kwa miaka miwili na imesitisha kulipa kodi ya 2012-2013
kwa barua ya Februari 3,2012 na kutoa maelezo kwenye barua kuwa
imefikia hatua hiyo kutokana na kuwapa wafanyakazi wake asilimia 15 ya
mishahara yao kulipa nyumba. Nyumba walionipangia ni ya vyumba viwili
na kodi iliyolipwa kwenye mkataba wa mwaka jana ni Milioni 4.8
Nilipatwa na mshutuko kidogo, nafsi ikanishauri niite menejiment
nyumbani tushauriane katika hili. Walikuja Machi 28, na wakanipa pole
ya kampuni tokea nirudi 2010 Shs 50,000. Lakini mazungumzo hayakuisha
kutokana na muda na kuahidi kurudi wiki inayofuata kwa mazungumzo
zaidi. Nimepewa notisi na mwenye nyumba April 23,2010.
Nadhani kutokana na kubanwa na kazi, hawakupata nafasi ya kurudi tena
kumalizia mazungumzo. Kwa mtazamo wa kifikira ni wazi msimamo ulibaki
palepale. Barua ya kusitisha kulipa kodi haikuja kwangu tu bali pia
mwenye nyumba alipata.
UFAFANUZI
Kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani Tanzania, Netcare Rehabilitation
Hospital, wanautaratibu mzuri sana. Kabla ya kuwa –discharged
wanakuruhusu ukae nje ya hospital kwa miezi mitatu, kama una mke au
mume na kama huna utatafutiwa nurse awe wa kike ama wa kiume mimi
nilipata nurse. Baada ya hapo una hudhuria mazoezi na vipimo kadhaa
kwa miezi mitatu. Ukifaulu kumaliza miezi mitatu wewe na mwangalizi
wako hasa wewe mgonjwa bila kupata matatizo, hapo wanaku-discharge.
Nilipiga simu kwa Katibu Kiongozi Ikulu wakati huo, Philemon Luhanjo
na kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii anahitajika
nurse kuja kukaa nami nje ya hospital kwa miezi mitatu, je
mtanisaidiaje? Kwa kweli jibu lao lilikuwa moja tu hatutatuma nurse
kutoka huku, tafuta huko huko, fedha za kumlipa, nyumba ya kulala,
chakula na usafiri, andika budget itume haraka tutalipa na wasiliana
na ubalozi waje kujua unakaa wapi na fedha zitatumwa ubalozini
watakuwa wanakuletea.
Nilipata nurse na miezi mitatu ilipokaribia kwisha nilifanya
mawasiliano kujua kama kutatumwa mtu wa kunifuata, wakanijibu njoo
naye huyo huyo watanzania waliofanikiwa kuangalia vyombo vya habari
wengi walimuona kwani nilirudi Mei 28, 2010. Baada ya mwezi alimaliza
mkataba name kutakiwa kutafuta nurse wa kukaa naye kwa saa 24 .
akapatikana na akafundishwa na M-South Africa jinsi ya kukaa na
mgonjwa wa Spinal Cord.
TSN, wakamlipa nurse wa South Africa Rand 12,500 alizokuwa anadai na
palepale nikauliza vipi kuhusu malipo ya nurse mpya ambaye ataachwa
na mimi? Kwa sababu serikali imemaliza jukumu lake na waliniambia kwa
kuwa wewe bado ni mwajiriwa wa TSN, jukumu lote sasa utakuwa chini yao
na ndiyo mmepewa pia jukumu la kumlipa kama mlivyofanya leo. TSN
walinijibu palepalekuwa suala la kumlipa nurse ni lako na familia yako
ila nyumba tutalipa.
Vodacom walijitokeza kubeba gharama za tiketi nilipopata ajali kwenda
Afrika Kusini na wasindikiaji wote, tiketi ya nurse niliyekuja naye.
Pia wakalipa tiketi yangu na nurse Desemba 8,2010 kwenda na kurudi
Afrika Kusini kwa ajili ya checkup.
Baada ya TSN kulipa nurse yule msouth afrika, nikawapigia Vodacom
Foundation kuwa nurse amemaliza mkataba na ameshalipwa fedha naomba
mumkatie tiketi. Hivyo ilikuwa Juni 25 na kesho yake Juni 26 2010
jioni wakaja watu wawili kutoka Vodacom Foundation na mmoja kutoka TSN
waliniambia wamekuja na vitu vitatu.
Wakamshukuru nurse kwa kazi nzuri , lakini wakamwambia , sisi ni
kutoka Vodacom. Vodacom Foundation inakuomba uendelee kumhudumia
Athumani . Na Vodacom watakulipa mshahara lakina tunaomba upunguze
kiwango.
Yule nurse akakubali akapunguza nusu ya mshahara aliokuwa akilipwa
na serikali. Wakamwambia sasa Vodacom Foundation inakata tiketi ya
kwenda nyumbani Afrika kusini kuaga. Akaomba siku 15, mkataba wa
mdomo ukakubaliwa na yule nurse na mshahara wa kwanza ukawa Julai 2010
kuendelea na kazi chini ya Vodacom. Julai 2010 wakamlipa.
Kilichoendela naomba nisiseme.
Muda wa checkup ulifika Desemba 2010, nikaitaarifu Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii. Wakakubali wakaandika barua kwa kugawa majukumu.
Afya wakasema watalipa gharama za matibabu, Vodacom tiketi za kwenda
na kurudi na TSN waliagizwa kulipa allowance kwa mgonjwa na nurse.
Tukasafiri Desemba 8,2010 na tukarudi Februari 28,2011. Malipo
yaliyofanywa na TSN kidogo ni aibu naomba nisiseme.
Hali hiyo ilinionyesha kuwa Vodacom Foundation walikuwa wanatambua
uwepo wa yule nurse. Lakini hadi nurse anaondoka alilipwa mshahara
mmoja tu na hata tiketi ya nurse kurudi Afrika Kusini Vodacom
hawakulipa.
Nililipa tiketi ya Business Class. Nikampa Rand 4,500 akakataa
akachukua Rand 2,500 tu , akaniambia, Athumani nakuacha katika hali
mbaya sana. Fuatilia haki zangu na zako, ukifanikiwa utaniambia na
Account ya benki , First bank nakuachia utaniwekea. Vodacom
Foundation hawajawahi kupokea simu yangu na Mkurugenzi wake hajawahi
kupokea simu yangu wala kuongea na mimi tokea nipate ajali.
Suala lingine waliniuliza nichague kitu kimoja, kujengewa nyumba
au kusomeshewa watoto. Mimi nilichagua kujengewa nyumba. Walichukua
chaguo langu. Tukamaliza mazungumzo.
Baada ya mwezi waliniambia suala lako limekubaliwa ila tumepata
Mkurugenzi mpya, lakini usijali. Mpaka hapa ninavyoongea danadana
ziliendelea mpaka ninavyoendelea kwenye nyumba, sijawahi tena kupata
jibu kutoka Vodacom. La mwisho nilijibiwa na mmoja wa watu wa Vodacom
Foundation aliniabmia wewe uliingia mkataba na kampuni ya One Plass na
si Vodacom Foundation.
SIKU YA LEO
Nimekuja leo kuutangazia umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa Account ya
CRDB ilikuwa maalumu kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka ya
Postal bank ambayo ya mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara
inayoingia benki ni 450,000
Nawalipa nurse, msaidizi wake na mfanyakazi 370,000. Maisha ya ulemavu
ni ghali sikutarajia . nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasa
la saba mwaka huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho yuko la pili.
Hawa wanasoma primary za kulipia wote hawa nawalipia 200,000 kila
mmoja kwa term jumla 400,000 hizo shule zina term nne kwa mwaka.
Gharama chakula, vifaa vya wanafunzi, gharama zao ndogondogo na za
kifamilia Pamoja na chakula kwa mwezi , inakwenda kati ya 750,000
mpaka 900,000 kwa mwezi.
Nimekuwa ombaomba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei
simu wala kujibu sms . siyo siri ndugu wote wamekimbia waliobaki ni
marafiki wa kweli wameniingiza katika familia zao. Hali yangu ni mbaya
sana kiuchumi.
Sina uwezo wa kulipa nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athumani
Hamisi, naomba watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na
ushauri wa madaktari walinishauri nisiishi mbali na mazingira ya
hospitali kulingana na hali yangu.
Makampuni , mashirika, wizara yoyote, shirika la nyumba la Taifa NHC,
watu binafsi, serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu
nawaomba wanisaidie kwa njia yoyote . kwa walio tayari naomba misaada
ipitie katika account No 01J2027048800 ya CRDB na Account No
010-00090488 ya Postal Bank
Kwa wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia M-pesa 0757 825 737,
Tigopesa 0655 531 188 na Airtel Money 0784 531 118; M-Pesa 0767 298
888 ya Chris Mahundi na Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru
Athumani Hamisi
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment