Saturday, 9 June 2012

[wanabidii] Bob Makani amefariki dunia

Tanzia Mohamed "Bob" Makani,
 
Atakumbukwa pia kama mmoja wa wanasheria mahiri waliowahi kutokea nchini ambapo aliweza hata kwenda na kitoroli kidogo cha kusukuma vitabu vya kwenda kumtoa kijasho mpinzani wake na jaji mahakamani. Aliwahi pia kuwa naibu gavana wa Benki Kuu kabla ya kuingia kwenye siasa za vyama vingi, na kuwa mmoja wa waanzilishi wa Chadema. Baada ya Edwin Mtei, ni Makani ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa pili wa Chadema ingawa wengi hawakumbuki hili. Wapuuzi wanaoneza udini nao huwa hawakumbuki kwamba Chadema imewahi kuongozwa na mwislamu kama makamu mwenyekiti na baadaye mwenyekiti. Alipotoka kwenye uenyekiti wa Chadema, ndipo Freeman Mbowe alipoingia. Kwa hakika Mohamed "Bob" Makani alikuwa mtumishi wa Tanzania kwa maana zote.
 
Apumzike kwa utulivu. Ameitumikia fani yake ya sheria; amelitumikia taifa pale Benki Kuu; ameitumikia demokrasia ya nchi yetu; sasa amelala.
 
Matinyi.
 

> Subject: [Mabadiliko ] Bob Makani amefariki Dunia.
> To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
> From: nicomedes76@gmail.com
> Date: Sat, 9 Jun 2012 20:06:56 +0000
>
> Taarifa zinasema amefia Agha Khan.
>
>
> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> This years motto: 'WALK THE TALK'
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en

0 comments:

Post a Comment