Friday, 8 June 2012

[wanabidii] MKAKATI WA KULINDA VYANZO VYA MAJI , MAJENGO NA MADARAJA

Kwa muda mrefu baadhi ya maeneo nyeti yanayounganisha nchi mikoa ,
miji , vijiji na hata vyanzo vingine vya maji na huduma nyingine
mbalimbali yamekuwa tupu bila ulinzi au kama ulinzi upo basi ulinzi
huo sio wa kutosha kwa kudhani tuko salama zaidi .

Kwa mfano Daraja la Ruvu na maeneo hayo kwa ujumla kumekuwa na uvamizi
wa wakulima na wafugaji mkubwa na maeneo mengi ya jirani sasa hivi
watu wanajenga na kuishi hata kutupa takataka na vitu vingine katika
mto huo ambao ndio chanzo kikuu cha maji kwa mji wa dare s
salaam .Ukipita Ruvu kumeandikwa tu usipige picha .

Ukija maeneo ya Dar es salaam kuanzia Daraja la Salenda ambalo zamani
liliwahi kupata matishio kadhaa ya kushambuliwa enzi za vita ya
ukombozi mwa kusini kwa afrika , Daraja la Jangwani katika mto
msimbazi , Daraja la Keko na lile la Kurasini .Madaraja yote haya
yanaunganisha sehemu kadhaa za jiji la dare s salaam pamoja .

nImetolea mfano wa Mkoa wa Dar es salaam kwa sababu ndio niliokuwa na
uzoefu nao sana , lakini kama unavyoona hapo maeneo hayo nyeti hayana
ulinzi wa kutosha wa mara kwa mara mpaka kufikia watu kuharibu
mazingira na miundombinu ya maeneo hayo na huko mbeleni hata wahalifu
haswa magaidi na maadui wengine wan chi yetu wanaweza kuhujumu
miundombinu hiyo .

Ni vizuri serikali kupitia wizara yake ya mambo ya ndani kuangalia
uwezekano wa kuanzisha ulinzi katika maeneo haya nyeti ya madaraja ,
vyanzo vya maji , viwanja vya ndege na walinzi wenyewe wapewe mafunzo
maalumu na pengine wawe na kitengo chao maalumu ndani ya wizara ya
mambo ya ndani ili kuweza kujiepusha kuingiliwa na wengine haswa
katika utendaji wao wa kila siku .

Kila mkoa unaweza kuwa na kitengo hichi ambacho kitafungiwa mashine za
mawasiliano ya kuweza kupata picha kwa mfumo wa CCTV na mengine ya
Digitali na kuweza kuchukuwa hatua za haraka na mapema .

Kama tuliweza kuwa na vitengo maalumu vya kupambana na Madawa ya
Kulevya , vya kupambana na Fujo inawezekana kabisa kuwa na njia hii ya
kulinda na sehemu zetu nyeti .

Kuna mifano kadhaa ya hujuma zilizowahi kufanywa dhidi ya sehemu hizi
siku za nyuma .

DARAJA LA SALENDA
Wakati wa Vita ya Ukombozi mwa nchi za Kusini mwa afrika majasusi wa
Afrika Kusini enzi hizo chini ya Utawala wa Weupe waliweza kufika
kwenye daraja hilo na kufanya vipimo na taarifa nyingine kwa ajili ya
kulipua daraja hilo pindi kiongozi akipita , lakini jaribio hilo
lilishindwa .

DARAJA LA MTO KAGERA
Ingawa baadhi ya watu wanasema ni wanajeshi wa Tanzania ndio walilipua
daraja hilo ili Nduli iddi amin asiweze kusonga mbele , taarifa
zinasema ni wanajeshi wa Nduli iddi amin ndio walilipua daraja hilo
baada ya kuingia ndani ya vijiji vya mkoa wa kagera na kuharibu mali .

Chonde chonde serikali ya Tanzania na wadau mbalimbali wa sekta ya
ulinzi lazima tuilinde nchi yetu kwa vifaa vya kisasa wakati huu ili
tuweze kujiepusha na hujuma zinazoweza kutokea siku za mbeleni .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment