Sunday, 10 June 2012

[wanabidii] JINSI YA KUSOMA VEMA NA KUFAULU KWA KIWANGO KIKUBWA SANA:

http://tanzaniaachievers.blogspot.com/
Nimekuwa naumia sana nikiona mwanafunzi yeyote yule akifeli mtihani
wowote ule wa darasani au chemsha bongo za kimataifa,maisha yangu ya
shule yalikuwa na furaha sana kwa sababunilikuwa sijui neno kufeli au
kuwa namba mbili darasani(shuleni kwangu kote) kwa mitihani ya kitaifa
na ndani ya shule.Kila muda nikiona kuna mwanafunzi anafeli naanza
kujaribu kuwa naye karibu ili naye aweze fanya vema awe kama mimi
Deogratius kilawe,kwa hakika nilifanikiwa sema kwa kiwango sio kikubwa
sana kutokana muda kuwa mdogo na miundo mbinu ya kuwafikia wanafunzi
wote wanapata haya matatizo ya kufeli au wanaofauli lakini hawajui
hata kwa nini wanafanafaulu na kufikiria ni kitu automatic kutoka
sehemu fulani na kuja kwao na siku wakianza feli wanasema kuwa
wamerogwa.Kama ilivyo kwa mafanikio mengine kufanikiwa ni juhudi
fulani mtu anazifanya ili mafanikio yatokee.Akili ina kazi nyingi moja
wapo ni kutunza taarifa,darasani ili uweze faulu inabidi uweze kuelewa
na kutunza taarifa kile ulichofundishwa na kutema kwenye karatasi ya
mtihani,sehemu hii kutunza kumbukumbu ndio sehemu ukurasa huu wa jinsi
ya kufaulu mtihani unahusika.Kadri unavyoweka juhudi ya kutunza vema
kumbukumbu ndio mafanikio darasani yanakuwa makubwa na sehemu
nyingine.Kama nilivyoeleza vema kwa topic ya jinsi ya kutunza
kumbukumbuku napenda kuenda moja vitu muhimu vya kumfanya mwanafunzi
afaulu:

(i)Manzingira akili ulivyo itengeneza,wewe unaonaje masomo?magumu au
marahisi?akili ni mjakazi wetu sisi wanadamu hutii kile sisi
tunachokiambia mfano kama unaona somo au masomo fulani magumu akili
hutii na kuamini hivyo,ukiamini kama masomo fulani au somo fulani ni
rahisi nayo hutii hivyo hivyo.Akili hubadilika kulingana na wewe
unavyobadilika.Sasa kama mwanafunzi weka mtizamo wako sasa sahihi,Kila
somo linawezekana,maraisi,hamna kitu hakiwezekani,kama ni mwanadamu
wenzako kaweka mfumo huo na katungua mawazo hayo kwa nini wewe
ushindwe?wote mna maasaa 24?wote mna lala na kuamka,wote mnakula na
kwenda haja,wote mnaweza kuwa na hudhuzi na furaha,kwa nini kitu
fulani aweze wewe uweze?basi nini wewe unatakiwa ubadilike,uanze amini
lazima ufanikiwe,maisha yanakupatia kile unawekea umakini kila siku.
(ii)Material manzuri,Lazima uwe na malighafi nzuri,dadisi material
gani wezako wanaofaulu wanayatumia,nenda kwa waliokutangulia mwaka wa
masomo uulize,tafuta material yaliyo marahisi kueleweka,kuna waandishi
wengine wa vitabu hupenda kufanya mambo kuwa magumu kwa kuandika mambo
mepesi sana kwa kutumia lugha ngumu sana ya zamani ili wapate umaarufu
na baadhi ya mashulei kuweka vitabu vyenye lugha ngumu sana kwa
maktaba zao na kupelekea wanafunzi kufeli mitihani yao,epuka waandishi
wanaotumia lugha ngumu hata yeye mwenyewe ukienda kumuuliza nini maana
neno fulani siku hiyo hadi aende kwa kamusi kutizama maana yake,Penda
kwenda kuchukua material kwa shule zenye ksifika kufaulisha vema,mimi
nilikuwa naenda kuchukua material mbambali kwa shule kama mirian
girls,st franscis,Maua seminari, mzumbe,nk Hakikisha kila aina la
tirio unalo,usikubali kuingia kwenda kufanya mtihani pasipo kupitia
mambo muhimu
(iii)Muda sio kila muda wa kusoma,kuna muda akili inaingiza taarifa
na kuhifadhi kwa haraka sana kuliko muda mwingine,Katika tafiti za
taasisi mbalimbali huu ndio muda ambayo ukisoma akili huhifadhi
taarifa kwa haraka kuliko muda wowote:

(a)Saa kumi usiku hadi saa nne asubuhi,ukisoma katika muda huu akili
huingiza taarifa na kuhifadhi kwa haraka kuliko muda wowote ule.

(b)Saa kumi jioni hadi saa nne usiku, Ukisoma katika muda huu akili
huingia taarifa kuliko muda wowote.

Kuanza kusoma usiku kucha ni kukosa maarifa,maana akili inamuda wake
wa kufanya kazi kwa ufanisi na baadae kuchoka na muda ambao huchoka ni
kuanzia saa tano asubuhi hadi saa kumi jion,na saa nne usiku hadi saa
kumi usiku ,katika muda huu hata kama ukilazimisha kusoma akili
kiwango cha kuingiza taarifaa ni kidogo sana na hivyo kuishia
kushindwa.
Umewahi sikia eti mtu fulani alikuwa anasoma sana lakini siku ya
mwisho akafeli?au umewahi sikia watu ambao wanasoma sana muda wote
lakini wanafeli sana darsani?umewasikia watu wanasoma muda wa mchana
na kukesha usiku na kuishia kupata maksi za wastani darasani?Ni kwa
sababu ya ku-time muda ganu akili inaingiza taarifa kuliko mwingine.

Huo muda mwingine unaweza tumia kwa kuingia madarasani na kumsikiliza
mwalimu na pia kufanya discussion.

(iv)Fanya kazi kwa juhudi na kuwa na mentor wako:Ili uweze fanikiwa
inabidi ufanye kazi kwa juhudi sana,lakini kwenye mfumo huu wa maisha
potote duniani ulivyotengenezwa inabidi mtu ili ufanye vema sana uwe
na mentor,mtu ambaye amefanikiwa na amekuzidi kidato au elimu,unapata
maelekezo yakeo ili na wewe uwe zaidi ya pale alipofika yeye.

http://tanzaniaachievers.blogspot.com

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment