Thursday, 7 June 2012

[wanabidii] UDINI NA UTANZANIA: TULIPOTOKA, TULIPO, TUELEKEAPO

Ndugu Watanzania mnaonaje iwapo mtajaribu kuachana na yaliyopita na muangalie ya leo na kesho. Ukweli ni kwamba yapo makosa mengi na mazuri mengi yaliyofanyika chini ya viongozi wetu wote, kuanzia kwa Mwl. Nyerere na mpaka hivi leo. Tuangalie hivi leo mambo gani yanaenda kiholelaholela. Iwapo tunaona makosa yanaendelea then tutafute ufumbuzi kiungwana ili tuweze kufanikisha malengo tunayoyaona yanafaa.
Sikweli kwamba sehemu fulani zilizotajwa ambazo wakazi wake wengi ni Waislamu watu hao hawapendi shule. Ukweli ni kwamba watu hao hawakuwa na uwezo au njia yoyote ya kuwapa elimu watoto wao. Waislamu pamoja na kuwa na elimu ndogo nyakati za ukoloni, ndio walikuwa mstari wa mbele katika juhudi zote za kusapoti uhuru wa Tanganyika kwani miji mingi ya Tanganyika ilikuwa inamilikiwa na waislamu as the majorities. Hata miji kama Moshi, Arusha ambako kuna wakristo wengi kimkoa, ma altown walikuwa waislamu. Kule Kigoma/Ujiji kulikuwa na sekondari moja tu kwa miaka mingi sana, wakati Kilimanjaro walikuwa na shule nyingi na wanazo nyingi na wataendelea kuwa nazo. Waziri wa elimu wa kwanza hayati ELIOFOO ndiye anaweza kulaumiwa kwa upendeleo huo. Baadhi ya wazazi waliojiweza kule Ujiji waliwapeleka watoto nje ili kupata elimu ya sekondaro. Miongoni wao ni kama SUNDAY MANARA ambaye alipelekwa na wazazi wakeUganda ili kupata elimu ya sekondari.
Kwa nini watu wanalalamika? Sababu ni kwamba tunaendelea kufanya makosa tuliayonza nayo. Hayo mambo ya Udini ni sababu tu ya kuonyesha jinsi watu kutopenda mambo mabaya yanayoendelea. Sidhani ni jambo zuri matatizo yote kuyaongelea kana kwamba DINI ndio chanzo chake. Kusema kwamba Malima aliteuliwa kuwa waziri ili atekeleze maslahi ya waislamu ni ujinga mkubwa sana. Ni sawa na kusema Eliofoo alizibadili shule kule Kilimanjaro ili ku promote wakristo. Iwapo tunaka mema kwa nchi yetu, achaneni na hizo historia za udini kwani wengi wetu tunajua yaliyofanyika na wengi waliyofanya hivyo leo hawapo hai au wadhifa wao umekwisha. Tunaweza kuwalaumu wakoloni kwani ndio waliojitahidi kufanya miganyiko hiyo kwa misingi ya kidini. Kwa uwezo wa Mungu hawakufanikiwa kwa percent mia ukilinganisha na nchi kama Nigeria ambapo mpaka leo tunayaona hayo matokeo ya mgawanyiko ya waingereza kwa manufaa yao na malkia wao. We must be one for good and bad.
Mtanganyika

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment