Kwa miaka ya karibuni watawala wetu wamekuwa na dhana potofu juu ya
shughuli na harakati za chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, kwa
nyakati tofauti tofauti viongozi wa serikali na wakuu wa chama tawala
wamekuwa wakikibatiza majina mbalimbali mabaya , mara chama cha
wahuni ,vibaka, wapenda fujo na watu wasioitakia amani nchi
hii,imefikia hata ikitokea wanachi wameanzisha maandamano kupinga
dhuruma fulani watawala wetu wakiulizwa chanzo cha vulugu hizo huwa
hawaumizi vichwa kutafuta chanzo bali wamekuwa wepesi wa kutoa majibu
mepesi kwa kusema vulugu hizo ni za kisiasa na zimeanzishwa na
kuratibiwa na wanachama wa CHADEMA, tumeona vulugu za Mbeya katika
soko la mwanjelwa mwishoni mwa mwaka jana kati ya wamachinga na polisi
ambapo roho za watu zilipotea,tumeshuhudia Songea pia mwanzoni mwa
mwaka huu ambapo wananchi waliandamana kupinga mauaji mbali mbali
yaliyokuwa yanafanywa na baadhi ya wananchi wasiokuwa na utu pasipo na
askari wetu kuchukua hatua zozote ingawa walikuwa wanapewa malalamiko
kuhusu mauaji hayo, katika mifano hiyo tu michache tulisikia watawala
wetu wakituaminisha kuwa vulugu zile zilikuwa za kisiasa na
zilianzishwa na wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Kwa upande mwingine wakuu wetu wa vyombo vya usalama nao wamekuwa
wakishutumiwa na viongozi wa CHADEMA kuwa wao ndio chanzo cha vulugu
mbalimbali zinazotokea kabla na baada ya mikutano ya CHADEMA, mfano
mkubwa hapa ni mikutano ya chadema iliyofanyika hivi karibuni katika
mji wa Arusha ambapo wanausalama wetu walilaumiwa kwa aidha kwa
kuchelewa kutoa vibali vya maandamano au kwa kutoa vibali
vinavyokanganya eti kwa sababu "intelijensia" inaonesha kuwa kutatokea
vulugu.
Jumamosi ya tarehe 26 mwezi huu wa tano viongozi na wanachama wa
CHADEMA wamefanya mkutano mkubwa wa amani katika viwanja vya jangwani
ambao pamoja na mambo mengine walizindua kauli mbiu yao mpya ya M4C
(Movement For Change) , Katika uzinduzi wa kauli mbiu hiyo Mwenyekiti
wa chama hicho aliwaambia wanachama kuwa lengo la M4C ni kupunguza
siasa za maandamano na kuanza kujiandaa kushika dola kwa kufanya
mikutano ya kawaida pande mbalimbali za nchi.
Watanzania wengi nikiwemo mimi mwenyewe walikuwa na wasiwasi na
hatima ya mkutano ule hasa kwa kuangalia mikutano mingi ya CHADEMA
ilivyoisha kwa vulugu kubwa na kuathiri maisha ya watu kwa namna moja
au nyingine,Lakini naomba nitumie nafasi hii kukipongeza Chama cha
Demokrasia na Maendeleo kwa kukubali sharti la kutokuandamana ingawa
ni haki yao ya msingi kikatiba, waliamua kujali maslahi ya watanzania
kwanza kuhofia vulugu kubwa ambayo ingeweza kutokea baada ya wao
kuandamana, nawaomba watanzania wote kwa ujumla bila kujali itikadi za
vyama tuwapongeze kwa hili kwani waliepusha shari kubwa ukizingatia
idadi ya watu waliohudhuria mkutano ule.
Pia naliomba jeshi la polisi liitishe mkutano wa wanahabari kama
kawaida yake na kukisafisha chama cha CHADEMA na kukibatiza majina
mengine ya kistaarabu kama chama chama cha wapenda amani, chama cha
wastaarabu na chama kinachoweka maslahi ya wananchi mbele kuliko kitu
kingine chochote kwani "Baniani mbaya lakini kiatu chake dawa"
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment